Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-MAUAJI

Mashitaka ya Azaria yaleta utengano kwa viongozi wa Israel

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amemuombea msamaha mwanajeshi wa Israel aliyekutwa na hatia ya kuuwa bila kukusudia baada ya kumpiga risasi raia wa Palestina aliyekutwa amelala chini akiwa na majeraha, na kubaini kwamba anaunga mkono wito wa msamaha kwa mwanajeshi huyo.

Wafuasi wa Sergeant Azaria mbele ya mahakama ya kijeshi mjini Tel Aviv, Januari 4, 2017.
Wafuasi wa Sergeant Azaria mbele ya mahakama ya kijeshi mjini Tel Aviv, Januari 4, 2017. REUTERS/Amir Cohen
Matangazo ya kibiashara

Kwa niaba ya majaji watatu, jaji Heller alisema hakukuwa na sababu yoyote kwa Azaria kufyatua risasi huku akijua fika raia huyo wa Palestina hakuwa hatari tena na imedhihirika kuwa mauaji hayo yalikua ni kitendo cha kulipiza kisasi.

Lakini viongozi mashuhuri katika Baraza la Mawaziri la Benjamin Netanyahu wamekosoa maamuzi hayo, lakini wazazi na ndugu wa raia huyo wa Palestina walisema maamuzi hayo yalikuwa yenye haki.

Jeshi limesema Sergeant Azaria amekiuka kanuni za maadili ya kijeshi lakini wanaomuunga mkono. Baadhi ya wanajeshi wa Israel wanasema mwanajeshi huyo alikuwa anajilinda na kwamba viongozi wake wamemgeuka.

Mwanajeshi huyo, Elor Azaria, kesi yake imekuwa ikisikilizwa kwenye mahakama ya kijeshi toka mwezi Mei mwaka jana, huku wanasiasa wa mrengo wa kulia wakionekana kumtetea licha ya viongozi wa juu wa jeshi kukosoa kitendo cha mwanajeshi huyo.

Adhabu dhidi ya mwanajeshi huyu inatarajiwa kutolewa katika siku chache zijazo, huku adhabu ya juu ya kosa alilotenda ikiwa ni kifungo cha miaka 20 jela.

Jaji kanali Maya Heller alitumia zaidi ya saa mbili na nusu kusoma uamuzi wa mahakama hiyo, akikosoa utetezi wa mawakili wa Azaria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.