Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: hali ya usalama yadhibitiwa baada ya shambulio

Shambulizi la watu wenye silaha dhidi ya jengo la shirika moja la kiutu mjini Kabul limemalizika na washambuliaji watatu wameuawa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan imesema Jumanne hii.

Moshi juu ya jengo la shirika la kiutu la Pamlarena lililolengwa na shambulizi la Jumanne Septemba 6, 2017.
Moshi juu ya jengo la shirika la kiutu la Pamlarena lililolengwa na shambulizi la Jumanne Septemba 6, 2017. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Watu arobaini na wawili ikiwa ni pamoja na wageni kumi wameokolewa," Msemaji wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan ameandika kwenye twitter, huku akithibitisha kifo cha mtu mmoja.

Kwa mujibu wa shirika la habri la AFP, shambulizi hili lilikua limelenga shirika moja la kiutu la Pamlarena, jina hilo likimaanisha "huduma" katika lugha ya Pachtoue. haijawekwa wazi kama shambulizihili kwa uhakika lilikua linalenga shirika la kihisani la Care International, ambalo pia jina lake lina maana ya "huduma" kwa Kiingereza. CARE International haijapatikana kwa sasa ili iweze kutoa maoni.

Shambulizi hili ni la tatu chini ya masaa 24 katika mji mkuu wa Afghanistan, baada ya mashambulio mawili yaliyowaua kwa uchache watu 24 na mamia kujeruhiwa Jumatatu wiki hii, mashambulizi yaliyodaiwa kutekelezwa na kundi la Taliban.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.