Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-USALAMA

Mtoto wa Osama bin Laden ataka kuuangusha utawala wa Kifalme

Hamza, mtoto wa Osama bin Laden, mwanzilishi wa al-Qaeda ametoa wito wa kuuangusha utawala wa kifalme nchini Saudi Arabia. Wito huu ameuelekeza hasa kwa vijana ambao wamechoshwa na utawala wa Kifalme nchini Saudi Arabia kujiunga na kundi la Al-Qaeda, mjini Yemen.

Hamza Bin Laden, mtoto wa Osama Bin Laden, katika video iliyorushwa mwezi Novemba 2001.
Hamza Bin Laden, mtoto wa Osama Bin Laden, katika video iliyorushwa mwezi Novemba 2001. AFP PHOTO/AL-JAZEERA
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa uhai wake, Osama Bin Laden alitaka kumfanya mtoto wake, Hamza, ambaye kwa leo ana umri wa miaka 23, mrithi wake katika uongozi wakundi la Al-Qaeda.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizothibitishwa, inaonekana kuwa Hamza bin Laden anasikilizwa na kuheshimiwa katika safu ya wanajihadi kuliko Ayman al-Zawahiri, mrithi wa baba yake tangu Mei 2011.

Tishio kwa Saudi Arabia na marekani

Mtoto aliyekua akipendwa sana na Osama bin Laden amewataka vijana wa Saudi Arabia, na wale wenye uwezo wa kupambana, kujiunga na kundi la AQPA lenye mafungamano na Al-Qaeda, lililoanzishwa mwaka 2009 kwa kuungana kati ya makundi mawili kutoka Saudi Arabia na nchini Yemen.

Miaka mitano baada ya kifo cha mratibu mkuu wa mashambulizi ya Septemba 11, 2001 nchini Marekani, jina la Bin Laden limeanza kusikika tena kama tishio la kweli kwa Saudi Arabia na Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.