Pata taarifa kuu
YEMEN-MASHAMBULIZI

Yemen: shule lashambuliwa kwa mabomu Haydan, watoto kumi wauawa

Shirika lisilo la kiserikali la Madaktari wasio na mipaka (MSF) limebaini Jumapili hii, Agosti 14, 2016 kwamba watoto wasiopungua kumi wa shule moja kijijini Haydan, nchini Yemen waliuawa Jumamosi hii katika mashambulizi ya anga ya muungano wa Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia.

Mtoto kutoka Yemen juu ya magofu ya nyumba katika mji mkuu wa Yemen unaodhibitiwa na waasi, Sanaa, Agosti 11, 2016.
Mtoto kutoka Yemen juu ya magofu ya nyumba katika mji mkuu wa Yemen unaodhibitiwa na waasi, Sanaa, Agosti 11, 2016. MOHAMMED HUWAIS / AFP
Matangazo ya kibiashara

hini ya miaka kumi na tano. Shirika la Umoja wa Mataifa linalotetea haki za watoto (UNICEF) limethibitisha taarifa hii, lakini jeshi la Saudi Arabia linasema mashambulizi ya muungano yamelenga kambi ya mafunzo ya waasi.

Shirika la habari la serikali la Saudi Arabia la SPA, limearifu kuwa muungano wa Kiarabu hivi karibuni umeshambulia " kituo cha mafunzo cha waasi" wa Huthi kaskazini mwa Yemen. Lakini msemaji wa wapiganaji wa Kishia, Mohammed Abdelsalam, amerusha kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook picha na video ambapo inaonekana miili ya watoto waliouawa ikifungwa katika blanketi.

Kwa mujibu wa MSF, mashambulizi yalifanyika Jumamosi katika eneo linalodhibitiwa na waasi katika kijiji cha Haydan, katika kaskazini magharibi mwa Yemen karibu na mpaka na Saudi Arabia. "Tuliona miili 10 a watoto waliouawa na 28 waliojeruhiwa, wote wakiwa na umri ulio chini ya mika kumi na tano na waliuawa katika mashambulizi ya muungano dhidi ya shule la dini ya kiislamu katika kijiji cha Haydan," amesema Malak Shaher, msemaji wa shirika la kibinadamu. Shirika la Umoja wa Mataifa linalotetea haki za watoto (UNICEF) limethibitisha taarifa hiyo, na kuongeza kuwa whanga walikuwa na umri wa miaka 6 hadi 14.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.