Pata taarifa kuu
UFARANSA-IRAQ-IS-UGAIDI

Jean-Yves Le Drian: Raqqa na Mosul "kudhibitiwa" mwaka 2016

Akiwa ziarani nchini Iraq, Waziri wa Ulizi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian, Jumatatu mjini Baghdad alijadili na viongozi waandamizi wa Iraq kuhusu uratibu wa mapambano dhidi ya kundi la Islamic State.

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian.
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian. REUTERS/Delmi Alvarez
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa ziara hii ambayo haikutangazwa, Waziri wa ulinzi wa Ufaransa pia alikitembelea kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa wanaotoa mafunzo kwa baadhi ya wanajeshi wa Iraq katika mapambano dhidi ya ugaidi. Kwa mujibu wa Jean-Yves Le Drian, "ngome za wanajihadi ya Raqqa nchini Syria na Mosul nchini Iraq zinapaswa kudhibitiwa mwaka huu."

Mpaka dakika ya mwisho, ziara hii ilikua katika usiri mkubwa. Jean-Yves Le Drian alitembelea Iraq siku chache tu baada ya ziara nyingine ya Rais wa Ufaransa, François Hollande, nchini Lebanon, Jordan na Misri.

Mjini Baghdad, Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa alikutana na mwenzake Khalid al-Obeidi, Waziri Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi, na Rais Fuad Masum.

Jean-Yves Le Drian alikuja kuihakikishia Iraq msaada wa Ufaransa katika vita dhidi ya kundi la Islamic State. Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa, mashambulio 582 yamelenga kundi la wanajihadi tangu mwezi Septemba 2014 kwa sehemu kubwa nchini Iraq.

Hivi karibuni, jeshi la Ufaransa linaendelea na jitihada zake kaskazini mwa nchi, katika Ukanda wa Mosul, na ule wa mlima wa Sindjhar lakini pia kusini zaidi katika Bonde la Mto.

Katika uwanja wa vita, jeshi la Iraq na wanamgambo wa Kishia wamelizuia kundi la Islamic State kusonga mbele, huku wakirejesha kwenye himaya ya serikali mji wa Ramadi, na sasa wanaendelea na mapigano kwenye kilomita kadhaa kutoka Mosul.

Pia WaziriLe Drian ametembea kituo maalumu cha jeshi dhidi ya ugaidi katika mji wa Baghdad ambapo mamia ya wanajeshi wa Ufaransayanatoa mafunzo na nasaha kwa jeshi la Iraq, hasa dhidi ya vilipuzi.

Kwa mujibu wa uongozi mkuu wa jeshi la Ufaransa, mwaka 2015 jeshi la Ufaransa lilitoa mafunzo kwa wanajeshi 3,700 (makomandoo) wa Iraq kwa jumla ya wanajeshi 18,600 waliopatishiwa mafunzo na muungano wa kimataifa dhidi ya IS unaoongozwa na Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.