Pata taarifa kuu
YEMENI-SAUDI-KUBADILISHANA WAFUNGWA

Yemen na Saudi Arabia wabadilishana wafungwa

Raia tisa kutoka Saudi Arabia "waliokua wanazuliwa Yemen" wameachiliwa huru dhidi ya raia 109 Kutoka Yemen waliokamatwa katika maeneo ya operesheni ya kijeshi karibu na mpaka wa kusini wa Saudi Arabia, mungano wa kijeshi wa Kiarabu umetangaza Jumatatu hii.

Raia wa Yemen wakikagua kiwanda cha Coca-Cola kilioharibiwa na mashambulizi ya muungano wa Kiarabu unaoongozwa na Saudia Arabia, jijini Sanaa Desemba 30, 2015.
Raia wa Yemen wakikagua kiwanda cha Coca-Cola kilioharibiwa na mashambulizi ya muungano wa Kiarabu unaoongozwa na Saudia Arabia, jijini Sanaa Desemba 30, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Muungano huu wa kijesi wa Kiarabu unapambana nchini Yemen dhidi ya waasi wa Kishia wa Huthi.

"Wafungwa tisa wa Saudi Arabia wamepokelewa na raia 109 wa Yemen waliokamatwa katika maeneo yaoperesheni za kijeshi" wamekabidhiwa kwa upande wa Yemen, muungano wa kijeshi wa Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia, umesema.

Zoezi hili la kubadilishana wafungwa, la pili la aina yake, limefanyika Jumapili hii, muungano umesema katika taarifa iliyochapishwa na shirika la habari la serikali ya Saudi Arabia la SPA.

Muungano huo haukueleza kuwa raia hao kutoka Saudi Arabia waliokua wakizuiliwa nchini Yemen ni wanajeshi au raia wa kawaida, na kama Wayemeni walioachiliwa huru ni waasi au raia wa kawaida.

Zoezi la kwanza la kubadilishana wafungwa lilitangazwa Machi 9, pamoja na mkataba wa usitishwaji wa mapigano kwenye mpaka wa Saudi Arabia na Yemen. Mwanajeshi wa cheo cha chini wa Saudi Arabia alikabidhiwa mamlaka ya nchi hiyo na Mashia saba waliweza kurejeshwa nchini Yemen.

Katika taarifa yake Jumatatu hii, muungano wa kijeshi wa Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia umesema kuwa zoezi la pili limefanyika kama sehemu ya mkataba wa usitishwaji wa mapigano.

Muungano huu umesema umeridhika na hali ya utulivu inayoshuhudiwa kwenye mpaka na kuwa na matumaini ya kuona hali hiyo "inasambaa katika maeneo ya vita, ili kuwezesha msafara wa magari yanayobeba misaada ya kibinadamu kuingia nchini Yemen na kuunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa kwa kufikia ufumbuzi wa kisiasa nchini Yemen kwa misingi ya azimio 2216 la Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.