Pata taarifa kuu
IRAQ-MASHAMBULIZI-USALAMA

Iraq: mashambulizi mawili yawaua watu 9 Baghdad

Kwa uchache watu tisa wameuawa Alhamisi hii katika mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga dhidi ya Msikiti wa Mashia, kaskazini-magharibi mwa mji wa Baghdad, polisi ya Iraq imesema.

Watu wakiwa katika eneo la shambulio, mashariki mwa mji wa Baghdad, Januari 11, 2016.
Watu wakiwa katika eneo la shambulio, mashariki mwa mji wa Baghdad, Januari 11, 2016. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Afisa wa polisi amesema kuwa "washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga ambao wamekua wamevalia mikanda ya kulipuka wamejilipua" mbele ya mahali pa ibada kwa Mashia katika wilaya ya Shula, na "kuua watu wasiopungua tisa na kujeruhi wengine 22, ikiwa ni pamoja na askari polisi polisi".

"Mshambuliaji wa kwanza wa kujitoa mhanga alijilipua kati ya waumini" waliokua wakitokea katika mahali pa ibada, shambulio ambalo "limeua na kujeruhi baadhi yao," amesema afisa huyo.

"Mlipuko wa pili umelenga vikosi vya polisi viliokua viliwasili katika eneo la tukio katika shughuli ya uokozi kwa watu waliojeruhiwa, shambulio hili limeua baadhi ya askari polisi," afisa huyo ameongeza.

Vyanzo vya hospitali vimethibitisha idadi hiyo ya watu waliouawa katika mashambulizi hayo mawili ya kujitoa mhanga. Mpaka sasa hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na mashambulizi.

Eneo la Shula ni ngome ya wapiganaji wa Mahdi, wanamgambo wa kiongozi wa Kishia Muqtada al-Sadr.

Mashambulizi haya yanatokea siku moja kabla ya maandamano yaliyoandaliwa na Sadr mjini Baghdad na ambayo amepania kushiriki mwenyewe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.