Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-MAUAJI

Askari polisi kumi wa Afghanistan wauawa

Mpiganaji mmoja wa kundi la Taliban aliejisajilisha kwa polisi wa mkoa unakabiliwa na mapigano wa Uruzgan, kusini mwa Afghanistan amewaua askari polisi 10 katika shambulio la pili kama hilo katika muda wa siku nane, chanzo kutoka serikali za mita kimebaini.

Vikosi vya usalama vya Afghanistan wakati wa mashambulizi yaliyotokea katika mji wa Mazar-i-Sharif, Afghanistan, Aprili 9, 2015.
Vikosi vya usalama vya Afghanistan wakati wa mashambulizi yaliyotokea katika mji wa Mazar-i-Sharif, Afghanistan, Aprili 9, 2015. AFP/AFP/
Matangazo ya kibiashara

Mtuhumiwa "aliwapa wenzake madawa ya kupoteza fahamu, kabla ya kuwaua, na kisha akatimka baada ya kuwaibia silaha zao", Dost Mohammad Nayab, msemaji wa mkuu wa mkoa wa Uruzgan, ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP. "Operesheni ya kumsaka imeanzishwa," amesema Rahimullah Khan, naibu mkuu wa polisi wa mkoa.

Kundi la Taliban, kupitia msemaji wake wa kawaida Zabiullah Mujahid, limekiri kuhusika na shambulio hilo ambalo limepelekea, amesema, wapiganaji kudhibiti eneo hilo ambapo walikua walitumwa askari polisi hao waliouawa.

Shambulio hili, ambalo limetokea katika wilaya ya Chinarto, ni sehemu ya mashambulizi makali yanayoendeshwa na kundi la Taliban nchini kote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.