Pata taarifa kuu
SYRIA-URUSI-AL QAEDA-MASHAMBULIZI

Syria: zaidi ya watu 39 wauawa katika mashambulizi ya Urusi

Watu wasiopungua 39 wameuawa Jumamosi hii katika mashambulizi ya anga ya ndege za Urusi dhidi ya jengo linalotumika kama gereza kwa kundi la al-Qaeda, kaskazini magharibi mwa Syria, kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali ambalo awali lilitoa idadi ya watu 10 waliouawa.

Ndege ya Urusi katika kambi ya jeshi la anga la Syria( picha ya video iliyotolewa na wizara ya Ulinzi ya Urusi), Oktoba 5.
Ndege ya Urusi katika kambi ya jeshi la anga la Syria( picha ya video iliyotolewa na wizara ya Ulinzi ya Urusi), Oktoba 5. REUTERS/Ministry of Defence of the Russian Federation/Handout
Matangazo ya kibiashara

"Kwa uchache watu 39 wameuawa na mashambulizi ya anga ya Urusi dhidi ya jengo linalotumiwa na kundi la Al-Nosra Front (tawi la Al Qaeda nchini Syria) kama gereza na mahakama katika mji wa Maaret al-Noomane", katika jimbo la Idleb, shirika la Haki za binadamu (OSDH) limesema.

"Wengi wa waathirika ni wafungwa, lakini pia kuna walinzi na raia watano, ikiwa ni pamoja na watoto, kwani kituo hicho kunakozuiliwa wafungwa wa al-Qaeda kiiko karibu na soko linalotembelwa na watu wengi", shirika la Haki za binadamu (OSDH) limeongeza.

OSDH imesema kuwa wengi wa wafungwa ni waasi wanaopinga kundi la Al-Nosra Front, na wakazi wanaishi pembezoni mwa gereza hilo walionyesha siku za nyuma kutoridhika kwao kwa sababu gereza hilo liko katika eneo lenye wakazi wengi.

Maaret al-Noomane ni mji muhimu kwenye barabara inayounganisha miji ya Damescus na Aleppo (kaskazini mwa Syria), unaodhibitiwa na waasi tangu mwishoni mwa mwaka 2012.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.