Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA. AJALI YA MOTO

Saudi Arabia: watu 25 wapoteza maisha katika ajali ya moto

Watu wasiopungua 25 wamepoteza maisha na wengine 107 wamejeruhiwa katika ajali ya moto uliyoharibu Alhamisi hii sehemu moja ya hospitali kusini magharibi mwa Saudi Arabia, Idara ya Ulinzi wa raia imetangaza.

Maafisa wa Zma Moto mbele ya Hopitali ya umma ya mji wa Jazan, Desemba 24, 2015.
Maafisa wa Zma Moto mbele ya Hopitali ya umma ya mji wa Jazan, Desemba 24, 2015. AFP/Saudi Civil Defence Directorate/AFP
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo imetokea katika wodi ya wagonjwa mahututi na wodi ya wazazi katika hospitali ya umma ya mji wa Jazan, Idara ya Ulinzi wa raia imesema kwenye Twitter.

Idara hiyo imebaini kwamba moto umedhibitiwa na kwamba "uchunguzi umeanzishwa ili kujua chanzo cha moto huo".

Idara ya Ulinzi wa raia imeongeza kuwa imehamasisha timu 21 ya maafisa wa Zima Moto na maafisa wa Idara ya dharura ili kudhibiti moto na kuokoa waathirika.

Operesheni ya maafisa wa Idara ya dharura imepelekea kuwaokoa watoto na wagonjwa mahututi waliokua wamelazwa katika vyumba mbalimbali vya wodi ya wagonjwa mahututi, lakini hata hivyo watu kadhaa wamepoteza maisha katika ajali hiyo, Wizara ya Afya imethibitisha kwenye Twitter.

Msemaji wa Idara ya Ulinzi wa raia, Yahia al-Qahtani, akinukuliwa na shirika la habari la serikali la SPA, amesema kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha imesalia 25 na 107 wamejeruhiwa, akiongeza kuwa Idara za huduma za dharura zimetolewa wito kuingilia kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.