Pata taarifa kuu
Syria-Urusi

Ndege za Urusi zashambulia ngome za wanajihad nchini Syria

Jeshi la anga la Urusi limefahamisha kwamba limelenga maeneo arobaini ya makundi ya kijihadi nchini Syria katika kipindi cha saa 24, huku wapiganaji wa kundi linalo jiita Islamic State likitowa wito wa kutekeleza mashambulizi ya kujitoa muhanga katika balozi za Urusi.

A frame grab taken from footage released by Russia's Defence Ministry October 5, 2015,
A frame grab taken from footage released by Russia's Defence Ministry October 5, 2015, Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na waziri wa ulinzi wa Urusi, idadi hiyo ya mashambulizi katika ngome za makundi ya kijihadi imepungua ukilinganisha na hapo awali.

Msemaji wa wizara ya ulinzi wa Urusi Igor Konachenkov amesema Ndege za kivita za Urusi zimefanya mashambulizi 41 yaliolenga maeneo 40 ya wapiganaji wa kijihadi katika mikoa ya Alepo kaskazini, Idleb kaskazini magharibi, Atakiyee kaskazini magharibi, Hama na Deir Ezzor.

Waziri huyo amefahamisha pia kwamba mashambulizi hayo yamelenga pia miundombinu ya wapiganaji wanaojiita Islamic State

Hapo jana jeshi hilo la Urusi lilitangaza kufanya mashambulizi 86, ikiwa ni idadi kubwa kufanywa na majeshi hayo tangu pale ilipoanza operesheni hizo Septemba 30 mwaka huu.

Igor Konachenkov amepongeza hatuwa iliofikiwa ya kubomolewa kwa ngome kuu ya uongozi wa kundi la Islamic State katika mji wa Deir Ezzor pamoja na ghala la silaha na kiwanda cha magari ambacho hutumiwa na wapiganaji wa Islamic State katika kutekeleza mashambulizi dhidi ya vikosi vya serikali ya rais Bashar al Assad.

Hayo yanajiri wakati huu kundi la Uslamic State likitowa wito kwa wanajihadi kutekeleza mashambulizi ya kujitoa muhanga na kulenga balozi za Urusi kokote duniani.

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.