Pata taarifa kuu
YEMENI-MASHAMBULIZI-USALAMA

Yemen. Mapigano katika mji wa Sanaa, mazungumzo ya amanji matatani

Vikosi vya serikali ya Yemen, vikisaidiwa na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia, vimeendesha operesheni kabambe dhidi ya waasi wanaoungwa mkono na Iran katikati mwa nchi hiyo, wakati ambapo mazungumzo ya kusaka amani yaliotangazwa na Umoja wa Mataifa yakionekana kuwa matatani.

Askari wa vikosi vinavyoinga mkono serikali, katika jimbo la Marib katikati mwa Yemen, Septemba 12, 2015.
Askari wa vikosi vinavyoinga mkono serikali, katika jimbo la Marib katikati mwa Yemen, Septemba 12, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Usiku wa Jumamosi kuamki Jumapil hii, utawala wa rais aliye ukimbizini Abd Rabbo Mansour Hadi umetangaza uamzi wake wa kutoshiriki katika mazungumzo ya aina yoyote wakati ambapo waasi wa Kishia wa Huthi watakua bado hawajaanza kuondoka katika maeneo wanayoshikilia tangu mwaka mmoja uliyopita, na kurejesha silaha walizokamata tangu walipoanzisha vita. Sharti ambalo linaonekana kuwa gumu kwa kukubali kwa upande wa waasi wa Huthi.

Masaa kadhaa baadaye, kiongozi wa kijeshi wa Yemen anayemuunga mkono Rais Hadi ametangaza kuanzishwa kwa mashambulizi dhidi ya ngome za waasi wa Huthi na washirika wao, ikiwani pamoja na kikosi cha wanajeshi ambao bado wanaendelea kumtii Rais wa zamani Ali Abdullah Saleh, katika jimbo la mafuta la Marib, mashariki mwa mji mkuu Sanaa.

" Mashambulizi haya ni makubwa na yana nguvu zaidi tangu kuanza kwa operesheni yetu ya kijeshi (mwezi Agosti) katika jimbo la Marib ", chanzo hihicho kimeliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.

Vikosi vya serikali vinaendesha mashambulizi kwa kutumia silaha za aina tofauti dhidi ya ngome za waasi katika maeneo ya Jufeinah, Faw na That-Alra "maeneo matatu ya kaskazini magharibi ya Marib, mji mkuu wa jimbo la Marib, kwenye barabara ya mji mkuu Sanaa, kimeongeza chanzo hicho.

Vikosi vya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia, ambavyo vimepeleka wanajeshi wa nchi kavu katika maeneo hayo wiki za hivi karibuni, “ wanatumia kwa sasa silaha za kivita katika operesheni hiyo ”, chanzo hicho kimeendelea.

Vikosi vya serikali ya Yemen, vinasaidiwa na helikopta za muungano unaoongozwa na Saudi Arabia na ndege za kivita.

Waasi wamethibitisha kupitia shirika la habri la SABA, ambalo wanamiliki, kwamba Jumapili hii wamerejesha nyuma mashambulizi ya majeshi ya serikali wanaosaidiwa na magari ya kijeshi na helikopta za Umoja wa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia katika mkoa wa Marib.

Lakini msemaji wa umoja huo, Brigedia Jenerali Ahmed Assiri, aliyehojiwa na runinga ya Al-Jazeera amebaini kwamba " operesheni bado ingali mwanzo ", akiongeza kuwa "inaendelea kulingana na plani iliyowekwa. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.