Pata taarifa kuu
YEMEN-MASHAMBULIZI-USALAMA

Yemen: nchi za Kiarabu zapeleka askari elfu kumi kwenye uwanja wa vita

Askari elfu kumi wametumwa kwenye uwanja wa mapambano nchini Yemen, uamzi ambo umechukuliwa na nchi za Kiarabu. Wanajeshi hao hao wataendesha vita vya nchi kavu dhidi ya waasi wa Kishia wa Huthi.

Magari ya kivita na mizinga ya majeshi ya nchi za Kiarabu katika Ghuba, Jumanne hii Septemba 8, 2015 katika mkoa wa Marib, kaskazini mwa Yemen.
Magari ya kivita na mizinga ya majeshi ya nchi za Kiarabu katika Ghuba, Jumanne hii Septemba 8, 2015 katika mkoa wa Marib, kaskazini mwa Yemen. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Hadi sasa muungano wa Kiarabu ukiongozwa na Saudi Arabia umeendelea kuridhika kusaidia jeshi linalomuunga mkono Rais Abd Rabbo Mansur hadi aliyekimbilia nchini Saudi Arabia, kwa kulipa silaha na kulisaidia kuendesha mashambulizi ya anga.

Inakisiwa kuwa askari hawa 10,000 watashiriki katika mashambulizi ya mji mkuu wa Sanaa, ambao bado unashikiliwa na wanamgambo wa Kishia.

Hakuna aliyefikiria kutumwa kwa askari hao 10,000 kwenye uwanja wa mapambano ambapo askari wengine 6,000 kutoka Misri na Sudan 6000 wataongezeka katika siku zijazo. Kikosi hiki cha askari wa nchi kavu kinaonyesha bila shaka taswira nyingine katika machafuko hayo yanayoendelea kushuhudiwa nchini Yemen kati ya Waarabu wa Kisuni na waasi wa Huthi wanaoungwa mkono na Iran.

Hayo yanajiri wakati ambapo katika miezi ya hivi karibuni Saudi Arabia walifutilia mbali uwezekano wa kuingilia kati kwa akari wa nchi kavu. Inaonekana kwamba vifo vya askari 60 wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Saudi Arabia, mwishoni mwa wiki iliyopita, vimetikisa nyoyo za viongozi kutoka nchi hizi.

Nchi za Kiarabu zinazoongozwa na Saudi Arabia zimeimarisha vikosi vyake vya ulinzi. Nchi hizi zimetuma vifaa vya ziada, ikiwa ni pamoja na helikopta 30, magari ya kivita na makombora.

Afisa mwandamizi wa Qatar amethibitisha Jumatatu wiki hii kuwa maelfu ya askari wa Qatar, ambao wamepewa vifaa vya kutosha, wamepiga kambi kwenye mpaka na Saudi Arabia na wanatarajiwa kuingia nchini Yemen katika siku zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.