Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-USALAMA

Afghanistan: Zaidi ya watu 40 wauawa katika mashambulizi ya Taliban

Kuanzia usiku wa Alhamisi hadi usiku wa Ijumaa wiki hii, katika mji wa Afghanistan, Kabul, kumeshuhudiwa mfululizo wa mashambulizi ya kujitoa mhanga na shambulio la mabomu yaliosababisha vifo vya watu 44 na mamia kujeruhiwa.

Mtu huyo (kwenye picha) anatafuta ndugu zake karibu na kambi yaIntegrity, Kambi ya kikosi maalum cha wanajeshi wa Marekani mjini Kabul. mfulilizo huo wa mashambulizi ulitokea usiku wa Ijumaa Agosti 7. Raia wanane waliuawa.
Mtu huyo (kwenye picha) anatafuta ndugu zake karibu na kambi yaIntegrity, Kambi ya kikosi maalum cha wanajeshi wa Marekani mjini Kabul. mfulilizo huo wa mashambulizi ulitokea usiku wa Ijumaa Agosti 7. Raia wanane waliuawa. AFP PHOTO/WAKIL K
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yametokea katika maeneo mbalimbali ya mji mkuu wa Afghanistan. Wapiganaji wa kundi la Taliban wamekiri kuhusika na mashambulizi hayo amabyo yamelenga vikosi vya usalama vya Afghanistan na Marekani.

Mawimbi ya muuaji yalioukumba mji wa Kabul tarehe 6 na 7 Agosti mwaka 2015 yanakuja zaidi ya wiki baada ya uteuzi wa kiongozi mpya wa kundi la Taliban, Mullah Mohammad Akhtar Mansour, na ameonekana kulaani kuanzishwa upya mazungumzo ya amani kwa muda mfupi kati ya kundi hilo la wanamgambo wa kiislam na serikali ya rais Ashraf Ghani.

Ijumaa usiku wiki hii, wakati wanafunzi wa shule la polisi walipokua wakirudi mwishoni mwa wiki, mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliyekua amevalia sare ya polisi, alijilipua katikati ya kundi lao. Kwa mujibu wa afisa mmoja wa polisi wa Afghanistan, akizungumza kwa masharti ya kutotajwa, shambulio la kujitoa mhanga, linalodaiwa na msemaji wa Taliban kutekelezwa na kundi lao, limewaua angalau watu 26 na kuwajeruhi wengine 28.

Masaa kadhaa baadaye, milipuko miwili ilisikika katika eneo la kaskazini ya uwanja wa ndege wa Kabul, karibu na kambi ya Integrity, kambi ya kikosi maalum cha wanajeshi wa Marekani. milipuko hiyo ilifuatiwa mara moja na milio ya risasi ya wapiganaji wa Taliban dhidi ya kambi hiyo. Mwanajeshi mmoja wa NATO na wapiganaji wawili wa Taliban waliuawa katika mapigano hayo, amesema Kanali Brian Tribus, afisa wa Marekani, ambaye ni mkurugenzi wa mahusiano ya umma kwa ujumbe wa NATO nchini Afghanistan (Resolute Support). Raia wanane pia waliuawa katika jaribio hilo la mashambulizi.

Usiku wote hadi asubuhi ya Jumamosi, Agosti 8, ndege za kivita na helikopta za vyombo vya usalama zimekua zikiruka katika anga ya mji mkuu wa Afghanistan, ambapo eneo nzima limekua limezingirwa.

Mashambulizi dhidi ya raia

Mfululizo huo wa shambulio la mabomu na mashambulizi ya kujitoa mhanga ulianza usiku wa Alhamisi hadi Ijumaa kwa mlipuko wa bomu lililokua limetegwa ndani ya lori karibu na eneo la jeshi katika eneo la Shah Shadid linalokaliwa na watu wengi, na kusababisha vifo vya watu 15 na wengine 248 kujeruhiwa. Inasemekana kuwa idadi hii inaweza kuongezeka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.