Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-USALAMA

Afghanistan: zaidi ya askari polisi 100 wajisalimisha

Jumamosi Julai 25 wapiganaji wa Taliban waliidhibiti kambi ya polisi ya afghanistan kaskazini mwa nchi hiyo, baada ya kujisalimisha kwa zaidi ya askari polisi mia moja, na kupelekea vikosi vya usalama vya Afghanistan kupata hasara kubwa tangu ujumbe wa kijeshi wa Nato uhitimishe majukumu yake nchini humo.

Wakati majadiliano yalikuwa yakiendelea katika mji wa Doha, Qatar, kati ya wawakilishi wa Taliban na serikali, mapigano kulitokea mapigano kaskazini ya Afghanistan, hapa ni katika jimbo la Kunduz, Mei 3, 2015.
Wakati majadiliano yalikuwa yakiendelea katika mji wa Doha, Qatar, kati ya wawakilishi wa Taliban na serikali, mapigano kulitokea mapigano kaskazini ya Afghanistan, hapa ni katika jimbo la Kunduz, Mei 3, 2015. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

" Zaidi ya askari polisi mia moja walipigana kwa siku tatu mfululizo. Walikuwa na silaha za kutosha na risasi kwa kuendelea na mapigano kwa muda wa miezi mitatu ", mkuu wa polisi wa jimbo la Badakhshan, jenerali Baba Jan, ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.

" Lakini walijasilimisha , baada ya (ya kuafikiwa) makubaliano na Taliban. Silaha zote na vifaa vingine vya kijeshi vilikamatwa na wapiganaji ", amesema Jenerali Baba Jan.

Kujisalimisha kwa askari polisi, kumetajwa na serikali ya jimbo hilo kuwa ni kitendo cha uhaini, kilichofanyika Jumamosi jioni katika wilaya ya Warduj katika jimbo la Badakhshan.

Naibu mkuu wa mkoa, Gul Muhammad Bedar, amesema kuwa kujisalimisha huko ni "kitendo kikubwa cha uhaini " ambacho itabidi kifanyiwe uchunguzi.

Askari polisi walishikiliwa kwamuda ufupi na wapiganaji wa Taliban kabla ya kuachiliwa huru, na baadhi yao waliwatuhumu hadharani viongozi wao kuwa " waliwasaliti " kwa kuhitimisha makubaliano na Taliban, kwa mujibu wa jenerali Baba Januari.

Msemaji wa kundi la Taliban Zabihullah Mujahid amesema katika taarifa kwamba askari polisi " waliachiliwa huru kwa sharti la kutojiunga na serikali ya Kabul ".

Sehemu hii inaonyesha tatizo la uaminifu wa baadhi ya majeshi ya Afghanistan, ambao walisambaratika katika mapigano mengi kutokana na ongezeko la mashambulizi ya waasi, licha ya rasimu ya mchakato wa amani.

Vikosi vya NATO vilihitimisha rasmu majukumu yao ya mapigano nchini Afghanistan mwezi Desemba mwaka jana, ambapo bado kunasalia baadhi ya wanajeshi 13,000 wa kigeni kwa kuyatolea mafunzo majeshi ya Afghanistan na kuendesha mapambano dhidi ya ugaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.