Pata taarifa kuu
Siku ya Watoto Duniani-Utumwa-Pakistan

Siku ya Watoto Duniani: watoto waendelea kukabiliwa na utumwa Pakistan

Novemba 20 ni Siku ya Watoto Duniani. Mwaka huu pia ni maadhimisho ya miaka 25 ya kutiwa saini Mkataba wa Haki za Mtoto. Pamoja na mafanikio makubwa, kazi bado kubwa katika nchi nyingi, ikiwa ni pamoja na Pakistan, ambapo watoto milioni 10 wanatumiwa katika shughuli mbalimbali, ukiwemo utumwa.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, watoto 3 kati ya 10 katika shule za msingi hawajakwenda shule nchini Pakistan.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, watoto 3 kati ya 10 katika shule za msingi hawajakwenda shule nchini Pakistan. REUTERS/Fayaz Aziz
Matangazo ya kibiashara

Watoto wengi nchini Pakistan, wanatumiwa kufanya shughuli mbalimbali, hususan katika viwanda, lakini pia katika mashamba na migodi. Raia milioni mbili wa Pakistan wanatumiwa kama watumwa, ikiwa ni pamoja na watoto wengi.

Mfumo huo umeendelea kushuhudiwa hadi sasa katika maeneo mengi nchini Pakistan. Wafanyakazi wamekua wakichukua madeni kwa waajiri wao ili waweze kulipa bili za matibabu au pia harusi, na kuendelea kulipa mzigo huo daima maisha yao yote. Hata vijana wamekua wakilazimishwa kuchangia kulipa madeni hayo.

Kwa mujibu wa Shirika la Global Slavery Index, watoto milioni 3.8 walio na umri uliyo chini ya miaka 14 nchini Pakistan wanatumiwa katika shughuli mbalimbali. Hali hii inaonesha idadi ya watoto ambao hawajakwenda shule. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, watoto 3 kati ya 10 katika shule za msingi hawajakwenda shule nchini Pakistan.

Pamoja na hayo, viongozi wanaendelea kupuuzia kupitisha sheria ya kuzuia ajira ya watoto, kama inavyoelezwa katika Katiba. Hata kama sheria ya kusitisha utumwa ilipitishwa katika miaka ya 1990 utumwa bado unaendelea kushuhudiwa nchini Pakistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.