Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAELI-Usalama

Wapalestina wawili wamchoma kisu raia wa Israel

Wapalestina wawili wamemuua kwa kisu Jumatatu Novemba 10 msichana wa Kiisrael na kumjeruhi askari mmoja katika mashambulizi mawili ambayo yamezidisha hali ya taharuki kuendelea kushuhudiwa katika aridhi za Palestina na Israel.

Katika eneo la tukio, ambapo mwanajeshi mmoja wa Israel alishambuliwa katika mji wa Tel-Aviv, Jumatatu Novemba 10.
Katika eneo la tukio, ambapo mwanajeshi mmoja wa Israel alishambuliwa katika mji wa Tel-Aviv, Jumatatu Novemba 10. REUTERS/Finbarr O'Reilly
Matangazo ya kibiashara

Shambulio la kwanza limetokea mchana karibu na kituo cha reli katika mji waTel Aviv, mji ambao kwa sasa unakabiliwa na machafuko. Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 17 amemchoma kisu askari mmoja wa Israel kabla ya kukamatwa katika jengo moja baada ya muda mfupi kufukuzana na polisi. Kijana huyo ni mkimbizi kutoka kambi ya wakimbizi ya Naplouse, kaskazini mwa mji wa Cisjordani unaokaliwa na walowezi wa Kiyahudi. Polisi imemtuhumu kijana huyo kwamba alikuwa aliingia Israeli kinyume cha sheria.

Saa tano baadaye, raia mwengine wa Palestina ameshambulia walowezi watatu wa Israel kwenye kituo cha mabasi karibu na mji wa Gush Etzion. Makaazi ya walowezi kusini mwa Jerusalim yamekua yakisababisha mvutano kuendelea. Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 25 alifariki na watu wawili wamejeruhiwa. Walinzi wa makaazi ya walowezi walimfyatulia risase kijana huyo na baadaye alifariki. Hii ni mara ya kwanza katika mzunguko wa sasa wa vurugu, ambapo utaratibu huu unatumika.

Jerusalem imekua ikishuhudia mashambulizi ya aina mbalimbali. Mashambulizi kwa kutumia gari yaliyoripotiwa hivi karibuni yalisababisha vifo vya watu wanne. Vijana wa Kipalestina waliohusika na mashambulizi hayo waliuawa na asikari polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.