Pata taarifa kuu
SYRIA-IRAQ-ISIL-Usalama

Syria: Taqba chini ya mamlaka ya taifa la kislamu

Wapiganaji wa kiislamu wanashikilia kwa sasa sehemu kubwa ya jimbo la Raqqa nchini Syria, baada ya kuuteka mji wa Taqba, kaskazini mwa Syria. 

Raia wa Tabqa washangilia kutekwa kwa mji wao na wapiganaji wa kiislamu, Agosti 24 mwaka 2014.
Raia wa Tabqa washangilia kutekwa kwa mji wao na wapiganaji wa kiislamu, Agosti 24 mwaka 2014. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa mambo ya nje wa Misri, Jordan, Qatar, Saudia Arabia, falme za kiarabu, wamekutana jana jumapili mjini Djeddah ili kutathimini hali ya machafuko inayoendelea nchini Syria na kuafikiana kuwasilisha matokeo ya mkutano kwenye jumuiya ya nchi za kiarabu.

Kutekwa kwa mji wa Taqba kutapelekea makundi hayo ya wapiganaji wa kiislamu, kuweka sawa wapiganaji wao, na huenda wakatumwa katika maeneo mengine hususan allepo, ambako wameanzisha mashambulizi kwa lengo la kuuteka mji huo. Wapiganaji hao wanapigana na jeshi la Syria, waasi wa Syria na wakurdi nchini Iraq.

Hayo yakijiri serikali ya Iraq imeomba msaada kwa jumuiya ya kimataifa wa kukabiliana na kundi la wapiganaji wa kijihadi Islamic State wanaoendeleza mauaji ya raia wasio na hatia nchini humo huku wakiendesha kampeni za kuung'oa madarakani utawala uliopo.

Kauli hiyo ya serikali ya Iraq inakuja wakati ikijaribu kujiimarisha baada ya wapiganaji hao wa kijihadi kuchua baadhi ya maeneo nchini humo licha ya kusaidiwa na marekani kukabiliana na kudi hilo la kigaidi.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Iraq Hoshyar Zebari amesema kuwa nchi yake inahitaji msaada wa jumuiya kimataifa ili iweze kukabiliana na kundi hilo na kwa msaada wa kila nchi unahitajika ili kukabiliana na ugaidi duniani kote.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya kigeni wa nchi jirani ya Iran, Mohammed Javad Zarif, akiwa ziarani nchini Iraq amesema kuwa Iran inauunga mkono jitihada za kutokomeza ugaidi na nchi yake iko tayari kusaidia Iraq japo kuwa suala hilo linapaswa kupewa kipaumbele na jumuiya ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.