Pata taarifa kuu
IRAQ-MAREKANI-ISIL-Usalama

Iraq: wapiganaji wa kislamu wapoteza eneo muhimu

Wapiganaji wa kikurdi wameweka kwenye himaya yao bwawa muhimu la kuzalisha umeme liliyoko Moussoul karibu na mji wa Erbil, kaskazini mwa Iraq, baada ya jeshi la Marekani kuendesha mashambulizi ya anga kwenye ngome za wapiganaji wa kislamu waliyokua wakishikilia eneo hilo.

Mmoja kati ya wapiganaji wa kikurdi akipiga doria kwenye milima ya Mossoul.
Mmoja kati ya wapiganaji wa kikurdi akipiga doria kwenye milima ya Mossoul. REUTERS/Azad Lashkari
Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji wa kikurdi (peshmerga), wakiendesha mashambulizi katika maeneo yanayoshikiliwa na wapiganaji wa kislam.
Wapiganaji wa kikurdi (peshmerga), wakiendesha mashambulizi katika maeneo yanayoshikiliwa na wapiganaji wa kislam. REUTERS/Stringer

Jeshi la Marekani linaendesha mashambulizi ya anga dhidi ya wapiganaji wa kislamu, baada ya Marekani kudai kwamba imekua ikilinda maslahi yake ncnini Iraq.

Ikulu ya Marekani imesema kwamba mashambulizi ya jeshi lake katika maeneo yanayoshikiliwa na wapiganaji wa kislamu hayatakoma iwapo wapiganaji hao hawatositisha harakati zao kuendelea na mapigano.

Jana jumapili jeshi la Marekani limeendesha mashambulizi ya anga 14, ambayo yaliharibu vibaya magari 10 ya wapiganaji wa kislamu na kuteketeza ngome yao.

Uongozi wa kijeshi nchini Marekani umefahamisha kwamba mashambulizi hayo dhidi ya wapiganaji wa kislamu yanalenga kuunga mkono jitihada za kufukisha misaada ya kibinadamu katika maeneo ambako imekua vigumu kufika kutokana na mapigano yanayoendeshwa na wapiganaji wa kislamu.

“Mashambulizi haya yanalinda miundo mbinu muhimu na wafanyakazi wa Marekani waishio Iraq pamoja na kuunga mkono jeshi, polisi na wapiganaji wa kikurdi kwa kuimarisha usalama nchini Iraq”, uongozi wa majeshi ya Marekani umesema katika tangazo uliyotoa.

Mapema jumamosi juma liliyopita, wapiganaji wa Peshmerga(ambao ni watu kutoka jamii ya Wakurdi wa Iraq) waliendesha mashambulizi kwa lengo la kudhibiti bwawa hilo muhimu, liliyokua likishikiliwa na wapiganaji wa kislamu tangu Agosti 7 mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.