Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-HAMAS-Siasa-Usalama

Jeshi la Israel laendelea na mashambulizi katika ukanda wa Gaza

Wanajeshi wa Israel kwa ushirikiano na vifaru na ndege za kivita wameendesha mashambulizi kwa siku ya pili leo ijumaa katika ukanda wa Gaza tangu waanzishe operesheni ya aridhini yenye lengo la kuvunja na kuteketeza silaha za Hamas, licha ya kuwa raia ndio wanaendelea kupoteza maisha.

Jeshi la Israel laendelea na mashambulizi ya aridhini katika ukanda wa Gaza, kwa siku ya leo Ijumaa, Jlai 18.
Jeshi la Israel laendelea na mashambulizi ya aridhini katika ukanda wa Gaza, kwa siku ya leo Ijumaa, Jlai 18. REUTERS/Nir Elias
Matangazo ya kibiashara

Wapalestina zaidi ya 23 wameuawa pamoja na mwanajeshi mmoja wa Israel tangu jana jioni wakati jeshi la Israel lilipoanzisha mashambulizi ya aridhini, licha ya wito unaotolewa na jumuiya ya kimataifa ya kusitisha mapigano kwa kuhofia maisha ya raia wa kawaida.

Mashambulizi yanayotekeltzwa na jeshi la Israel katika ukanda wa Gaza.
Mashambulizi yanayotekeltzwa na jeshi la Israel katika ukanda wa Gaza. REUTERS/Mohammed Salem

Mapigano hayo yanaendelea kushuhudiwa kusini mwa Palestina, hususan katika miji ya Khan Younès na Rafah, pamoja na kaskazini karibu na mpaka wa Israel. Njia moja ambayo imekuwa imebaki, ambayo raia wamekuwa wakitumia imefungwa.

Wakaazi wengi wa mji wa Gaza wameyahama makaazi yao, huku jeshi la Israel likiendelea na mashambulizi ya aridhini. Wakati huo huo wanajeshi wa Israel wameanza kushambulia ngome za Hamas ambazo ziko chini ya aridhi ambako kundi hlo inaaminiwa kuwa wamekua wakipitisha biashara na kuigiza silaha.

Hata hivo, Hamas imesema kwamba Israel itakiona cha mtima kuni.
“Israel inaendelea kupoteza muda, kuona imeshindwa katika mashambulizi yake ya anga na majini, haitafaulu chochote katika mashambulizi haya ya aridhini, bali itakiona cha mtima kuni”, amesma kiongozi wa Hamas, Khaled Mechaal.

Hata hivo Norway imesema kitendo cha Israel cha kuendesha mashambulizi ya aridhini siku moja baada ya kusitisha mapigano hakikubalikii, wakati jitihanda za kusitisha mapigano zilikua hazijagonga mwamba.

“Ninaona kwamba ni jambo lisilokubalika kuona Israel inaanzisha mashambulizi ya aridhini, wakati kulikua na imani ya kusitisha mapigano”, waziri wa mambo ya nje wa Norway, Boerge Brende, ameiambia televisheni ya TV2 Nyhetskanalen ya Norway.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.