Pata taarifa kuu
GAZA-ISRAELI-HAMAS-Usalama-Mkataba

Gaza : matumaini ya maelewano iwapo mkataba utaheshimishwa

Serikali ya Israel na Mamlaka ya Palestina wametangaza kukubaliana na ombi la Umoja wa Mataifa la kusitisha mapigano baina yao kwa muda wa saa tano alhamisi wiki hii kuruhusu kuwasili kwa misaada ya kibinadamu wakati ambapo mashambulizi ya Ukanda wa Gaza yakiendelea.

Makubaliano ya usitishwaji mapigano yatekelezwa katika ukanda wa Gaza.
Makubaliano ya usitishwaji mapigano yatekelezwa katika ukanda wa Gaza. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Wakati hayo yakijiri, Jumuiya ya kimataifa inapendekeza kutuma ujumbe wa kimataifa katika harakati za kumaliza mashambulizi hayo, jambo ambalo nchi ya Misri inaonekana kuafikiana nalo, kama alivyobainisha waziri wa mambo ya Nje wa Ufaransa Laurent Fabius, .

Baada ya ombi la umoja wa mataifa jeshi la Israel limesema kuwa litasitisha mashambulizi kati ya saa nne asubuhi hadi saa tisa kwa saa za Gaza, ili kuwaruhusu wakaazi kupata chakula na huduma muhimu.

Wakati huo huo Israel na Hamas wamekubaliana kusitisha mapigano, ili kuwaruhusu wakaazi wa ukanda wa Gaza kupata chakula.

Makubalianao hayo ya usitishwaji mapigano yameanza kutekelezwa tangu saa nne saa za Gaza na Isarael sawa na saa moja saa za kimataifa. Mkataba huo ni ombi la Umoja wa Mataifa kwa kuwafikishia misaada ya chakula wakaazi wa ukanda wa Gaza.

Hata hivo, zaidi ya wapelestina thelathini wameuawa mapema alhamisi hii asubuhi kabla ya utekelezaji wa mkataba huo wa usitishwaji mapigano. Huenda uheshimishwaji wa mkataba huu ukafungua njia ya mazungumzo kati ya Israel na Hamas na

Wakaazi wa ukanda Gaza waendelea kupoteza ndugu zao kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel.
Wakaazi wa ukanda Gaza waendelea kupoteza ndugu zao kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel. REUTERS/Mohammed Talatene

kupelekea mapigano yanasitishwa moja kwa moja.

Jeshi la aridhini la Israeli
Jeshi la aridhini la Israeli REUTERS/Finbarr O'Reilly

Israel imejikubalisha kuheshimu makubaliano haya ikibaini kwamba iwapo Hamas itathubutu kurusha makombora katika aridhi ya Israel, jeshi lake halitosita kujibu haraka iwezekanavyo mashambulizi hayo. Wanajeshi wa ziada 8000 wako tayari kukabiliana na mashambulizi yatakayoendeshwa na Hamas.

Katika uwanja wa mapigano, mashambulizi ya anga ya jeshi la Israel yameendelea katka ukanda wa Gaza huku wapiganaji wa Hamas wakiendelea kurusha makombora katika aridhi ya Israel. Lakina inaarifiwa kuwa hali ya utulivu imeshuhudiwa usiku wa kuamkia leo alhamisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.