Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAELI-HAMAS-Usalama

Palestina: Hamas yakiri kurusha maroketi katika aridhi ya Israeli

Kundi la Hamas limekiri kuhusika katika mashambulizi ya maroketi katika mji wa jerusalem na tela Aviv ikiwa ni jibu la mashambulizi ya anga yalioanazishwa na vikosi vya Israeli yaliogharimu maisha ya watu 28.

Mpiganaji wa tawi la kijeshi la Hamas,  Ezzedine al Qassam, kusini mwa Gaza.
Mpiganaji wa tawi la kijeshi la Hamas, Ezzedine al Qassam, kusini mwa Gaza. (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Duru kutoka katika ukanda wa Gaza zimearifu kuwa watu 24 wamepoteza maisha wakiwemo wanawake wawili na watoto watano kufuatia mashambulizi ya anga yaliotekelezwa na vikosi vya Israeli. Mbali na hayo vikosi vya Israeli vimewauwa wafuasi wanne wa kundi la Hamas walioshambuli kituo kimoja kilichopo kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Duru za kitabibu zimeeleza kuwa watu zaidi ya 150 wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo.

Katika taarifa iliotolewa na tawi la kijeshi la kundi la Hamas Ezzedine Al Qassam , kundi hilo limeshambulia miji ya Haifa , Jerusalam na tel Aviv.

Kikosi cha wapiganaji wa tawi lakieshi la Hamas.
Kikosi cha wapiganaji wa tawi lakieshi la Hamas. REUTERS/Mohammed Salem

Duru kutoka Israeli hazijadhibitisha mashambulizi ya mji wa Haifa, lakini jeshi limethibitisha kutokea kwa mashambulizi katika mji wa Handera kwenye umbali wa kilometa 100 kaskazini mwa Gaza.

Kengele za tahadhari zimesikika kwa mara ya kwanza kaskazini mwa Tel Aviv kwenye umbali wa kilometa 60 kaskazini mwa ukanda wa Gaza

Katika hatuwa nyingine, kundi la watu sita waliokamatwa na polisi nchini Israeli kwa kushukiwa kuhusika na kifo cha kijana mmoja wa kipalestina, wamekiri kuhusika na mauaji ya kijana huyo aliuawa kwa kuchomwa moto akiwa hai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.