Serikali ya Sudan Kusini, ikiongozwa mrengo wa rais Salva Kiiri inasiistiza kwamba uchaguzi utafanyika disemba mwaka ujao licha ya mrengo wa makamo wa kwanza wa rais Reik Machar, kuonesha kutorithia wazo hilo.
Machar na wabunge wanaoegemea wapande wake wanataka mkataba wa amani wa mwaka 2018 kutekelezwa vikamilifu kabla ya uchaguzi huo kufanyika, ikiwemo kuundwa kwa katiba na kunganisha vikosi vya jeshi.
katika Makala haya wachambuzi wa siasa za Kimataifa, Lugete Mussa Lugete, ambaye pia ni mwanahostoria kutoka nchini Tanzania pamoja na dkt Braine Wanyama, mchammbuzi wa siasa za kimataifa na mhadhiri katika chuo kikuu cha Kibabi kinachopatikana Bungoma, nchini Kenya.