Pata taarifa kuu
Wimbi la Siasa

Mapigano mashariki mwa DRC.

Imechapishwa:

Makala hii imeangazia hali ya usalama inayojiri huko mashariki ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, ambako Kundi la waasi wa M23 likiungwa mkono na Rwanda lilifanikiwa kuyateka miji miwili muhimu ya Rutshuru na Kiwanja mashariki ya DRC na kuendelea na mapigano kwenye viunga vya mliji hiyo, huku serikali ya Kinshasa ikichukua uamuzi wa kumfurusha Balozi wa Rwanda nchini humo, Vincent Karega huku Juhudi za kimataifa zikiendelea kuzipatanisha nchi hizo mbili.Kuangazia hili tumewaalika profesa Pacifique Malonga, ni mtaalamu wa sias aza Rwanda akiwa jijini Kigali nchini Rwanda naye Guerschom Kahebe ni mchambuzi na mtaalamu wa siasa za DRC akiwa Calfornia nchini Marekani.

Wakaazi wa Goma, Jimboni Kivu Kaskazini, walijitokeza barabarani kuandamana wakipinga mapigano yanayofanywa na waasi wa M23 na kuishutumu Rwanda kwa kuunga mkono kundi hilo lenye silaha. Hapa, waandamanaji walichoma bendera ya Rwanda mnamo Oktoba 30, 2022.
Wakaazi wa Goma, Jimboni Kivu Kaskazini, walijitokeza barabarani kuandamana wakipinga mapigano yanayofanywa na waasi wa M23 na kuishutumu Rwanda kwa kuunga mkono kundi hilo lenye silaha. Hapa, waandamanaji walichoma bendera ya Rwanda mnamo Oktoba 30, 2022. AP - Justin Katumwa
Vipindi vingine
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.