Kupandikiza au kuhamisha viungo vya mwili kama njia mojawapo ya matibabu inazidi kushika kasi .Mataifa mengi yanafanya upandikizaji wa figo ,moyo ,ini ,Cornea na sehemu za umme.
Matangazo ya kibiashara
Kuna hata hivyo changamoto katika hili,mataifa bado hayana sheria za kutosha kusimamia zoezi hili. Kwa sasa upandikizaji unafanyika kwa watu wanaohusiana huku kukiwa na hitaji kubwa ya viungo muhimu vya mwili.Hii ni kutokana na kuwepo wagonjwa wengi wanaopata viungo vyao muhimu vimefeli kutokana nao kuwa na magonjwa yasiyoambukizwa.