Kuipa hedhi heshima kama haki ya msingi miongoni mwa wanawake
Imechapishwa:
Cheza - 09:28
Umaskini umechangia wasichana wengi kukosa Sodo na kushindwa kwenda shule
Ukosefu wa sodo ndio umeonekana kuchangia wasichana wengi nchini Kenya kutoudhuria shule hasa maeneo ya mashinani.Utamaduni pamoja na ufukara ndivyo vimeonekana kuchangia halii hii kwa asilimia kubwa.
Utafiti uliofanywa na shirika la Borgen, asilimia 65 ya wasichana na wanawake nchini kenya hukumbwa na ukosefu wa sodo hivyo kuathiri masomo na shughuli zao za kila siku.
Lakini hata hivyo katika kaunti ya kwale ,idadi ya wasichana imeanza kuongezeka shuleni baada ya jamii pamoja na mashirika mbalimbali kuanzisha mpango wa ugavi wa sodo kwa wasichana.