Ulimwengu huadhimisha siku ya malaria kila tarehe 25 mwezi wa nne. Malaria ni ugonjwa wa kuambukiza ambao unaenezwa na mbu wa jenasi anayefahamika kama Anopheles na kusababishwa na kidubini aina ya Plasmodium.
Kulingana na shirika la afya duniani Nigeria inasajili visa hivyo kwa asilimia 31.3, DRC asilimia 12.3,Tanzania kwa asilimia 4.1 na Niger kwa asilimia 3.9.
Vilevile Kulingana na ripoti ya shirika la maendeleo ya Ufaransa nchini Kenya AFD ni kwamba Kisumu inaongoza kwa visa vya malaria kwa hadi asilimia 40.
Na Kwenye makala haya tunazungumzia ugonjwa huu na jinsi ya kupambana nao. Nimezungumza nae Peris Oloo ambae anaugua malaria na anaelezea baadhi ya dalili alizokua nazo.kisha Daktari anaezungumzia Ugonjwa huu kwa kina na jinsi mtu anaeza uepuka.