Pata taarifa kuu
Siha Njema

Jinsi mabadiliko ya tabia nchi yanavyoathiri afya na haki za akina mama

Imechapishwa:

Mabadiliko ya tabia nchi yameendelea kufifiza usalama wa chakula chenye lishe,kupunguza uwezo wa akina mama wanaotegemea kilimo asili kulisha familia zao na kuongeza idadi ya magonjwa yasiyoambukizwa

Bi Nancy Rono mkulima wa Wimbi kaunti ya Bomet nchini Kenya
Bi Nancy Rono mkulima wa Wimbi kaunti ya Bomet nchini Kenya © Carol Korir
Matangazo ya kibiashara

Kwenye makala haya tunaangazia kilimo cha wimbi ambacho japo ni cha asili,ni chakula chenye lishe na kinachohitajika kwa sasa kwa ajili ya wagonjwa wa kisukari.Kupungua kwa uzalishaji wa wimbi kutokana na ukame,gharama ya juu ya mbegu na mashamba yanayotumika kwa mara ya kwanza ,yamechangia akina mama wengi hawawezi kuwalisha familia zao kwa kuwa wimbi ni kipato cha wanawake,inatumika kuwalisha watoto na watu wenye umri uliokwenda wengi wao wakiwa wanauguza ugonjwa wa kisukari.

Tunaangazia vile vile kilimo cha sasa cha wimbi ambacho wanawake katika kaunti ya Bomet ,kusini mwa bonde la ufa ,nchini Kenya wamebidi kukumbatia ili kuendelea na kilimo cha wimbi wakati huu ulimwengu unapokumbwa na athari haasi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Vipindi vingine
  • 10:20
  • 08:40
  • 10:25
  • 10:09
  • 09:55
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.