Pata taarifa kuu
Afrika Ya Mashariki

Ndoa za utotoni zinavyo sababisha fistula Afrika Mashariki

Imechapishwa:

Ndoa za utotoni zinatajwa kusababisha athari kwa watoto wa kike kisaikolojia, kiafya, kiuchumi na hata Kwenda mbali zaidi kusabisha athari za afya

Ramani ya nchi za EAC
Ramani ya nchi za EAC © EAC.int
Matangazo ya kibiashara

Kuzidi kushadidi kwa ndoa za utotoni katika mataifa ya ukanda wa Afrika mashariki utajwa moja ya kisababisha kwa binti kupata ugonjwa wa fistula ya uzazi ambayo upatikana wakati wa kujifungua.

Fistula ya uzazi inachangia asilimia 8 ya vifo vya uzazi, na asilimia 90 ya visa vya kujifungua watoto wafu huku wataalamu wakieleza kuwa watoto wa kike waliopo kwenye ndoa za utotoni wapo hatarini zaidi kupata ugonjwa huo.

Zubeda Maulidi mwenye umri wa miaka 18 sasa siyo jina lake halisi mkazi wa Meatu mkoani Simiyu,aliolewa akiwa na umri wa miaka 17 kasoro huku mumewe akiwa na umri wa miaka 21 anasema alikatisha masomo mara baada ya kuhitimu darasa la saba na kutumbukia katika ndoa za utotoni

Inakadiriwa kuwa wanawake na wasichana 500,000 katika nchi zaidi ya 55 za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Asia na Pasifiki, nchi za Kiarabu, Amerika Kusini na Caribbea wanakadiriwa kuishi na fistula, huku maelfu zaidi ya visa vipya hutokea kila mwaka

Vipindi vingine
  • 09:59
  • 09:59
  • 09:59
  • 09:59
  • 09:59
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.