Pata taarifa kuu

Viongozi wa Serikali ya Israeli waitaka Jumuiya ya Kimataifa kutoiondolea vikwazo Israeli hadi pale itapoweka wazi mpango wake wa Nyuklia

Viongozi wakuu wa Israel wamesema kwamba nchi ya Iran itahukumiwa kwa vitendo vyake na wala sio kwa kauli zake kuhusu mpango wake wa Nyuklia. Kauli hii inakuja siku moja baada ya majadiliano ya siku mbili baina ya Iran na mataifa yenye nguvu juu ya Nyuklia ya Iran.

Benjamin Netanyahu
Benjamin Netanyahu France 24
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wameitaka Jumuiya ya Kimataifa kuendelea kuiwekea vikwazo Iran kwa muda wote hatuwa madhubuti zitakuwa hazijachukuliwa kuhusu mpango huo, na kukumbusha kwamba Iran inaendelea kukiuka azimio la Umoja wa Mataifa unaoitaka kusitisha na kuachana na mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium.

Wakati wa mazungumzo ya juzi na jana mjini Geneva kati ya Iran na mataifa yaneye nguvu, ikiwa ni pamoja na Marekani, China, Rusia, Uingereza, Ujerumani na Iran, serikali ya Teheran ilikubali mpango wa kufanyiwa ukaguzi wa kushtukiza kwa mpango wake wa Nyuklia, ombi lililotolewa na Marekani.

Marekani imepongeza hatuwa hiyo iliofikiwa na kuitaka Iran kuzamilia zaidi katika mazungumzo yajayo ya Novemba 7 na 8

Siku ya Jumanne na Jumatani ujumbe wa Iran uliwasilisha mapendekezo yake mapya kuhusu mpango wake wa Nyuklia mpango ambao mataifa ya magharibi yanasema wataendelea kuutazama licha ya kuridhishwa na baadhi ya mapendekezo.

Catherine Ashton mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya EU ambaye alikuwa anaongoza ujumbe wa mataifa mengine ya Ulaya, amesema ameridhishwa na hatua waliyofikia mpaka sasa.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema kuwa wamekubaliana na nchi nyingine kimsingi na kwamba wanamatumaini ya kufikia muafaka kwenye vikao vijavyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.