Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Maelfu ya raia wa Zimbabwe hawakupiga kura kwenye uchaguzi wa 31July2013

Watu wanaokadiriwa kufikia laki tatu na elfu hamsini wanaelezwa kushindwa kupiga kura nchini Zimbabwe huku wengine zaidi ya laki mbili na elfu sitini wakielezwa kusaidiwa kupiga kura na maofisa wa tume ya taifa ya uchaguzi kwenye uchaguzi uliofanyika juma moja lililopita. 

Wananchi wa Zimbabwe waliojitokeza kwenye zoezi la kupiga kura kwenye uchaguzi wa tarehe 31July2013, baadhi yao walishindwa kupiga kura
Wananchi wa Zimbabwe waliojitokeza kwenye zoezi la kupiga kura kwenye uchaguzi wa tarehe 31July2013, baadhi yao walishindwa kupiga kura Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na tume ya taifa ya uchaguzi nchini Zimbabwe ZEC, zimeonesha kuwa watu milioni 3.5 walipiga kura kwenye uchaguzi wa tarehe 31 ya mwezi July mwaka huu na kusaidia kumuongezea muhula wa saba rais Robert Mugabe.

Kwenye taarifa ya tume ya taifa ya uchaguzi ZEC, inaongeza kuwa raia wanaokadiriwa kufikia elfu sitini na nne mia nne na themanini na tatu hawakupiga kura kwasababu walirudishwa nyumbani kutokana na sababu mbalimbali mjini Harare.

Tatizo la kuwepo kwa idadi kubwa ya wananchi walioshindwa kupiga kura kwenye uchaguzi wa mwaka huu pia liliripotiwa na waangalizi wa kimataifa walioko nchini Zimbabwe huku wao wakiwa bado hawajaweka idadi kamili ya watu ambao hawakupoga kura lakini duru zinasema inakadiriwa kuwa ni watu zaidi ya milioni moja.

Maeneo ambayo yanaonesha rais Mugabe kujinyakulia kura nyingi ni kwenye maeneo ya vijijini ambako ndiko ambako chama tawala cha ZANU-PF kina nguvu kubwa na hivyo kwa sehemu kubwa kukiangusha chama kikuu cha upinzani nchini humo cha MDC-T kinachoongozwa na waziri mkuu Morgan Tsvangirai.

Kwenye maeneo mengi ya vijijini pia kuliripotiwa raia wengi kushindwa kupiga kura baada ya kuzuiliwa na maofisa wa tume ya taifa ya uchaguzi kutokana na majina ya waliowengi kukosekana kwenye orodha ya wapiga kura ama kudaiwa kujiandikisha kwenye vituo vingine.

Hata hivyo uchaguzi wa mwaka huu uligubikwa na mizengwe mingi huku waangalizi huru wakisisitiza kuwa orodha ya wapiga kura ilichakachuliwa ili kukibeba chama tawala cha ZANU-PF.

Asilimia 99.97 ya wapiga kura waliokop kwenye maeneo ya vijijini walijiandikisha kupiga kura huku aslimia 67.94 wakijiandikisha kupiga kura kwenye maeneo ya mijini hali ambayo pia iliibusha maswali mengi kuhusu uwazi wa uchaguzi wa mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.