Pata taarifa kuu
ROME-VATICAN

Papa Francis kutumia sikukuu ya Pasaka kuosha miguu wafungwa na kutembelea wasiojiweza

Katika kile kinachoonekana ni kuendeleza utamaduni wake, kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis Alhamisi hii anashiriki kuwaosha miguu wafungwa watoto wanaoshikiliwa kwenye magereza nchini humo. 

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa na ikulu ya Vatican, imesema kuwa Papa Francis amelenga kuendelea na utamaduni wake wa kuwa karibu na wananchi na kwamba wakati wa kujiandaa na sikukuu ya Pasaka ameamua kutembelea magereza.

Hatua hiyo ya Papa inaendana kinyume na utamaduni wa kanisa hilo ambapo imezoeleka kumuona kiongozi huyo akifanya maandalizi ya Pasaka akiwa katika kanisa la mtakatifu Lateran Basilica.

Kiongozi huyo ametaka kuwepo mabadiliko ya kiroho kila siku kwa waumini wa kanisa hilo hasa kwa kuwaombea na kuwasaidia wale ambao wana uhitaji ili kutimiza maoenzi ya Mungu kwa watu wake.

Papa Francis ameonekana kuwashangaza wengi kutokana na misimamo yake ambapo ni juma hili tu, amekataa kuishi kwenye Ikulu ya Vatican na badala yake ataishi kwenye nyumba za wageni ambazo ziko jirani na kanisa hilo.

Kwa mujibu wa msemaji wa Vatican ratiba ya Papa kwa sikukuu ya Pasaka itakuwa ni kutembea kwenye mitaa ya mji wa Rome na kuzungumza na wananchi wa kawaida pamoja na kutembelea magereza zaidi kutimiza matakwa ya kiroho kama kiongozi wa kanisa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.