Pata taarifa kuu
UN-MAREKANI

Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kuchunguza operesheni za mashambulizi ya ndege zisizo na rubani

Ofisi ya tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa UN imetangaza kuanzisha uchunguzi rasmi kuhusu mashambulizi ya anga yanyofanywa na ndege maalumu ambazo hazina rubani kwenye operesheni mbalimbali duniani. 

Moja ya ndege ambazo hazitumii rubani
Moja ya ndege ambazo hazitumii rubani Reuters
Matangazo ya kibiashara

Tume hiyo imesema kuwa kuanza kuchunguza operesheni za mashambulizi ya ndege hizo kunakuja kufuatia tuhuma kuwa huenda mashambulizi hayo yamesababisha kuwepo kwa makosa ya uhalifu wa kivita ambapo maelfu ya watu wasio na hatia wameripotiwa kuuawa kutokana na mashambulizi hayo.

Be Emmerson ambaye ni muangalizi wa tume hiyo ya Umoja wa Mataifa ndiye aliyetangaza kuanza kwa uchunguzi huo siku ya alhamisi kufuatia maombi ya Serikali ya Urusi, Pakistan na China ambazo zimetaka kuchunguza ufanisi wa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotiwa saini na mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja huo Navi Pillay, imesema kuwa kutafanyika uchunguzi wa kina na wakimaabara kubaini iwapo mashambulizi hayo yamekuwa yakilenga makazi ya watu na kusababisha mauaji ya halaiki kwenye baadhi ya maeneo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa lengo la uchunguzi huo pia unalenga kulishauri baraza la usalama la Umoja huo kuchukua hatua madhubuti kudhibiti mashambulizi hayo iwapo kutakuwa na matokeo ya kwamba kumekiukwa haki za binadamu wakati wa mashambulizi hayo.

Tume hiyo imeongeza kuwa uchunguzi wake haulengi taifa lolote na watu wasitake kutafsiri kuwa unalenga taifa la Marekani, Uingereza wala Ujerumani ambazo zimekuwa zikitumia ndege zisizo na rubani kuteketeza ngome za wapiganaji wa Al-Qaeda na wale wa Taliban.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.