Juhudi za kuwakomboa Wafanyakazi wa kigeni waliotekwa nchini Algeria zaendelea huku Operesheni ya Jeshi la Ufaransa nchini Mali yachanja mbuga
Imechapishwa:
Cheza - 19:37
Utekaji wa Wafanyakazi wa Kigeni wanaofanyakazi katika Kiwanda cha Gesi nchini Algeria umeendelea kuzua maswali mengi huku juhudi mbalimbali zikifanywa kwa lengo la kuwakomboa kutoka kwenye makucha ya Wanamgambo wa Kiislam, Jeshi la Ufaransa limeendelea kuongeza idadi ya wajeshi wake nchini Mali kuendelea na mchakato wa kuyasambaratisha Makundi ya Kiislam wenye Msimamo Mkali wanaoshikilia eneo la Kaskazini, Serikali ya DRC yakataa pendekezo la Kundi la Waasi la M23 la kutaka iundwe serikali ya mpito kama njia moja wapo ya kupata suluhu kwenye eneo la Mashariki na Wananchi wa Kenya wamejitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi la kupiga kura kuchagua wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi March mwaka huu!!