Pata taarifa kuu
Syria-Uturuki

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lakashifu Syria kwa kuishambulia Uturuki

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekashifu shambulizi la Syria nchini Uturuki lililosababisha vifo vya watu watano mjini Akcakale, shambulizi ambalo baraza hilo linasema linatishia usalama katika kanda ya Mashariki ya Kati.

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa Baraza hilo wamesema ni wazi kuwa machafuko nchini Syria kwa kiasi kikubwa huenda yakasabisha nchi zingine kama Uturuki kuathiriwa na machafuko hayo ikiwa hatua za dhahrura hazitachukuliwa.

Bunge nchini Uturuki siku ya Alhamisi  lilipitisha mswada wa kuruhusu majeshi yake kuivamia Syria katika mpaka wake ikiwa serikali italamizimika kufanya hivyo kutokana na mashambulizi ya makombora yaliyorushwa  na majeshi ya Syria nchini Uturuki na kusababisha vifo vya watu watano yataendelea.

Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan  amesema hatua ya wabunge kupitisha mswada huo haimanishi kuwa Uturuki inaingia vitani na Syria bali hatua za kijeshi zitachukuliwa dhidi ya serikali ya Damascus kwa kipindi cha mwaka mmoja ikiwa serikali itaona hatua hiyo inastahili.

Siku ya Jumatano Uturuki ilipiza kisasi kwa kurusha makombora yake nchini Syria na kusababisha mauaji ya wanajeshi wa serikali kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Syria.

Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ulianza kutetereka mwezi Juni baada ya Syria kudungua ndege ya kijeshi ya Uturuki na kusababisha vifo ya marubani wake.

Uturuki imeendelea kuituhumu Syria kwa kutoheshimu sheria za kimataifa kwa kuingia katika mipaka yake na kusababisha mashambulizi jambo ambalo Uturuki inasema haitavumilia tena.

Uongozi wa majeshi ya kimataifa NATO, yameshtumu hatua hiyo ya Syria na kuongeza kuwa itaendelea kusimama na serikali ya Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.