Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Marekani yathibitisha kumuua Abu Yahya al-Libi kiongozi wa pili wa Al-Qaeda

Marekani inasema shambulizi la ndege zake za kivita zisozokuwa na rubani limemuua Abu Yahya al-Libi kiongozi wa pili wa kundi la kigaidi duniani la Al-Qaeda.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali ya Marekani, Jay Carney amesema Washington imethibitisha kuuawa kwa al Libi ambaye mwaka 2009 pia aliripotiwa kuuliwa na majeshi ya Marekani.

Hata hivyo Pakistan ambayo imekuwa ikipinga mashambulizi ya Marekani katika himaya yake ,haijathibitisha kuuawa kwa Al-Libi .

Shambulizi hilo lilitokea katika mpaka wa Pakistan na Afganistan na kusababisha kuuawa kwa zaidi ya watu 10 akiwemo al Libi ambaye amekuwa akilengwa kwa muda mrefu.

Marekani inaamini kuwa kuuawa kwa Osama Bin Laden,mwaka uliopita sasa Libi ndiye wa pili katika uongozi wa al qaeda baada ya Ayman al Zawahiri raia wa Misri kuchukua uongozi wa kundi hilo.

Al Libi anaripotiwa kuwa msimamizi wa oparesheni za kila siku nchini Pakistan.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.