Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-USALAMA

Ngazi za juu katika serikali ya Kenya zakumbwa na mvutano

Mvutano bado unaendelea kuripotiwa kati ya rais Uhuru Kenyatta na makamu wake, William Ruto. Mvutano huo unahusiana na uchaguzi ujao wa urais mwaka 2022.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kulia) na Makamu wa rais Williame Ruto
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kulia) na Makamu wa rais Williame Ruto Yasuyoshi CHIBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ingawa kampeni bado haijaanza, wafuasi wa kambi zote mbili tayari wamekuwa wanaendelea kukabiliana bila huruma kwa miezi kadhaa. Tayari, vurugu zinaibuka kati ya koo zinazopingana. Utulivu wa nchi unaweza kukumbwa na hali ya sintofahamu.

Jumapili ni siku Misa. Hapa misa inamaanisha mikutano ya kisiasa. Jumapili, kiongozi wa zamani wa upinzani Raila Odinga, ambaye sasa amejiunga na rais wa sasa, aliwapokea wafanyabiosaha wakuu maarufu nchini.

Walakini, mkutano wa makamu wa rais William Ruto, ulipigwa marufuku na mamlaka, ikibaini kwamba ni katika hali ya kuimarisha usalama wa nchi. Uamuzi ambao umesababisha ukoo wa Ruto kiupandwa na hasira.

Sintofahamu inaendelea kuripotiwa katika ngazi za juu serikali nchini Kenya kwa miezi kadhaa. Rais Kenyatta ataondoka madarakani mwaka 2022. Alitarajiwa kumuunga mkono makamu wake wa Williamo Ruto kulingana na mkataba walioafikiana. Lakini Uhuru Kenyatta, inadaiwa kuwa ameanza kumtafuta mrithi wake mwingine.

Tangu wakati huo, Ruto amejitenga. Miaka 2 kabla ya uchaguzi, tayari ameanza kuhamasisha kambi yake na kutoa jumbe za uhasama dhidi ya ukoo wa Kenyatta. Matokeo: kambi hizo mbili zimekuwa zikishambuliana, hadi kusababisha vifo. Siku chache zilizopita, maandamano ya kisiasa yaligeuka kuwa machafuko na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 2.

Viongozi wa nchi hiyo wana wasiwasi: "Ikiwa hakuna kinachofanyika kwa sasa kutuliza hali ya mambo, Kenya inaweza kuingia kwenye machafuko." Hali inayofanana na ile ya mwaka 2007, wakati vurugu za baada ya uchaguzi zlisababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.