Pata taarifa kuu
BURUNDI-UFARANSA-USHIRIKIANO

Ufaransa yarejesha ushirikiano na Burundi katika sekta ya ulinzi

Wakati nchi ya Burundi ikiwa chini ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya tangu mwaka 2015 pale rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza alipoamua kuwania muhula wa 3, na kukataa kuzungumza na wapinzani waliopo nje ya taifa hilo, serikali ya Ufaransa imetangaza kurejesha ushirikiano wake na Burundi katika sekta ya ulinzi.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza Juni 7, 2018.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza Juni 7, 2018. © REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa inaonekana imeamua kuchukuwa hatua hiyo peke yake, kwa kuanzisha kutoa upya msaada wake wa moja kwa moja kwa Burundi tangu mwanzoni mwa mwaka 2019, kwa matumaini hasa ya kuimarisha uchumi ambao unaelezwa kufikia kiwango cha chini kabisa.

Ushirikiano huu ni katika lengo la kuinua uchumi na uelewano wa kisiasa katika nchi hiyo  ambayo inaelezwa kuwa inaendelea kuvunja haki za binadamu kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu.

Hatua hii ya Ufaransa kutoa msaada kwa Burundi ilichukuliwa wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Ezekiel Nibigira, mjini Paris mwezi Oktoba mwaka jana.

Taarifa hii ilitolewa na balozi wa Ufaransa nchini Burundi Laurent Delahousse, siku mbili kabla ya maadhimisho ya uhuru wa Ufaransa Julai 14 mwaka huu.

Hatua hii inakuja wakati Umoja wa Ulaya umeongeza muda wa vikwazo kwa Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.