Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-BAJETI-FEDHA-USALAMA

Wabunge nchini Sudan Kusini wakwamisha Bajeti ya serikali

Wabunge nchini Sudan Kusini wamezuia kupitishwa kwa bajeti ya fedha ya mwaka 2019/2020 kwa sababu wanajeshi na wafanyikazi wengine wa serikali, hawajalipwa kwa miezi kadhaa sasa.

Spika wa bunge nchini Sudan Kusini akisikiliza wabunge wakati wa kusomwa kwa Bajeti ya fedha Juni 19 2019
Spika wa bunge nchini Sudan Kusini akisikiliza wabunge wakati wa kusomwa kwa Bajeti ya fedha Juni 19 2019 eyeradio.org
Matangazo ya kibiashara

Serikali nchini humo ilikuwa imependekeza matumizi ya Pauni za nchi hiyo Bilioni 208, sawa na Dola za Marekani Bilioni 1.3 kwa matumizi ya miradi mbalimbali.

Miongoni mwa miradi ambayo ilikuwa imelengwa kufadhiliwa kutumia bajeti hiyo ni pamoja na maendeleo ya miundo mbinu kama ujenzi wa barabara miongoni mwa miradi mbalimbali.

Spika wa bunge Lino Makana alilazimika kusitisha kikao cha bunge, baada ya wabunge kuapa kuwa, wasingeweza kuendelea kujadili na kupitisha  bajeti hiyo hadi pale wafanyikazi watakapolipwa mishahara yao.

“Wanajeshi wetu wanalamizika kukata miti ili kuchoma mkaa kwa ajili ya kupata fedha za kuendesha maisha yao, inawezekana vipi tunashindwa kuwalipa wafanyikazi wanofanya kazi katika mabalozi yetu kwa mwake ,” ? aliuliza Mbunge Elizabeth Adut.

“Walimu wetu hawalipwi, wanafunzi hawafundishwi kwa sababu walimu wameamua kujitafutia kazi katika mashirika ya kibinafsi, ili kukimu maisha yao,” aliongeza mbunge huyo.

Mapigano yaliyoanza nchini humo mwaka 2013, yameendelea kudhoofisha usalama na siasa za nchi hiyo, huku viongozi wakuu rais Salva Kiir na mpinzani wake Riek Machar wakishindwa kutekeleza mikataba kadhaa ya amani.

Kiir na Machar wanatarajiwa kuunda serikali ya mpito, baadaye mwaka huu, baada ya makubaliano waliyokubaliana mwaka 2018 jijini Khartoum nchini Sudan.

Sudan Kusini ilipata uhuru wake mwaka 2011, baada ya kujitenga na Sudan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.