Pata taarifa kuu
TANZANIA-MAREKANI-USALAMA-ONYO

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania watoa taarifa ya kiusalama

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, umetoa taarifa ya kiusalama katika maeneo yanayotembelewa na wageni katika jiji la kibiashara la nchi hiyo la  Dar es salaam.

Nembo ya serikali ya Marekani
Nembo ya serikali ya Marekani tz.usembassy.gov
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa kupitia tovuti ya Ubalozi huo, imeeleza kuwa kuna uvumi huenda mashambulizi hayo yakalenga mtaa wa kifahari wa Masaki, Hoteli ya Serena, Slipway na maeneo ya Msasani.

Hata hivyo, Ubalozi unasema hauna ushahidi wa kutokea kwa mashambulizi hayo, lakini unatoa wito wa watu kuwa makini na kuepuka mikusanyiko wa watu wengi.

Mkuu wa jeshi la Polisi nchini humo Simon Sirro amesema anafahamu kuhusu uvumi huo na maafisa wa usalama wanazifanyia kazi.

Tanzania haijawahi kulengwa na visa vya mashambulizi katika miaka ya hivi karibuni, isipokuwa mwaka 1998, wakati magaidi wa al-Qaeda waliposhambulia Ubalozi wa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu 11.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.