Pata taarifa kuu
BURUNDIUN-HAKI

Umoja wa Mataifa waongeza mwaka mmoja kwa Tume ya Uchunguzi nchini Burundi

Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu limeamua kuongeza muda wa mwaka mmoja kwa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi nchini Burundi, wakati serikali ya Bujumbura ilikuwa imetishia kujitoa kwenye taasisi hiyo.

Askari wasambaratisha umati wa watu katika wilaya ya Cibitoke, Bujumbura, Burundi, Mei 7, 2015.
Askari wasambaratisha umati wa watu katika wilaya ya Cibitoke, Bujumbura, Burundi, Mei 7, 2015. © AP
Matangazo ya kibiashara

Azimio hilo, lililopendekezwa na Umoja wa Ulaya, lilipitishwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa mataifa kwa kura 23 kwa jumla ya nchi 47 ambazo zina wajumbe kwenye Baraza hilo. Nchi saba zilipinga azimio hilo na nchi 17 zilijizuia kupiga kura.

Katika ripoti iliyochapishwa tarehe 5 Septemba, Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kwamba ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na uhalifu dhidi ya ubinadamu umeendelea bila hofu yoyote nchini Burundi mwaka 2017 na 2018, vitendo ambayo vinatekelezwa hasa na idara ya Upelelezi (SNR), polisi na jeshi bila kusahau kundi la vijana kutoka chama tawala CNDD-FDD, Imbonerakure.

Azimio hilo "linalaani vitendo vyote vya vurugu vinavyoendelea kutekelezwa nchini Burundi na pande zote, au na watu " na kuamua kuongeza muda wa mwaka mmoja kwa Tume hiyo "ili iweze kuendelea na kuchunguza kwa kina."

Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi, Doudou diene, amekaribisha katika taarifa uamuzi wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

Tume hii iliundwa mnamo mwaka 2016 na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, lakini serikali ya Burundi kamwe kuijairuhusu kuingia nchini humo, hadi kutishia maafisa wa uchunguzi kwamba itawafungulia mashitaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.