Pata taarifa kuu
KENYA-IMF-UCHUMI

Wabunge watumia nguvu kupitisha ushuru mpya wa mafuta Kenya

Wabunge nchini Kenya wamepitisha pendekezo la rais Uhuru Kenyatta kuongeza kodi ya asilimia nane kwa bidhaa za mafuta nchini humo kutoka asilimia 16.

Kisima cha mafuta Kaskazini Magharibi mwa Turkana, Kenya (Picha ya kumbukumbu).
Kisima cha mafuta Kaskazini Magharibi mwa Turkana, Kenya (Picha ya kumbukumbu). AFP/HO/Tullow Oil PLC
Matangazo ya kibiashara

Ilimlazimu Spika wa Bunge Justin Muturi na kiongozi wa walio wengi katika bunge hilo Aden Duale, kutumia nguvu kupitisha pendekezo hilo baada ya kuonekana kuwa wabunge wengi wa chama tawala na upinzani, walikuwa wamekataa pendekezo hilo ambalo litasabisha kupanda kwa gharama ya maisha.

Tarehe 1 Septemba ushuru tata wa asilimia 16 kwenye bidhaa ya mafuta ulianza kutumika. Ushuru huu ulisababisha bei ya mafuta ya gari kupanda, huku bei ya nauli ya usafiri na bei za baadhi ya bidhaa zikipanda mara dufu.

Kutokana na hali hiyo Wakenya wengi walipandwa na hasira. Rais Kenyatta ilimbidi apendekeza kupunguza 8% kwenye ushuru huo uliokuwa ulipitishwa.

Kabla ya ushuru huo kupitishwa kulikuwa na hali ya sintofahamu bungeni, huku baadhi ya wabunge wakiondoka nje na kususia kikao hicho cha bunge. Mashahidi wanasema baadhi ya wabunge walivunja utaratibu wa shughuli za bunge, huku wakipiga kelele "sifuri! sifuri! wakiomba ushuru huo kufutwa moja kwa moja.

Wabunge waliopinga ushuru huo walikuwa ni wenye hasira. Mmoja wao amezungumzia kikao hicho cha bunge kuwa ni cha "aibu" na ameahidi kufikisha malalamiko yao mahakamani. Mwingine ametishia kumtimua kwenye nafasi yake Spika wa bunge.

Kwa kushuru huu, serikali inatarajia kurejesha dola Milioni 170, ambazo ni mara mbili kama ushuru ungelikuwa umesalia kwenye 16%.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.