Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-SIASA-USALAMA

Riek Machar akataa kusaini mkataba wa amani Sudan Kusini

Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar, amekataa kutia saini mkataba wa amani na serikali, mkataba ambao ulikua na lengo la kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vingi nchini humo.

Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini Riek Machar akihudhuria zoezi la kutia saini mmkataba wa amani na serikali ya Sudan Kusini huko Khartoum, Sudan, Juni 27, 2018.
Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini Riek Machar akihudhuria zoezi la kutia saini mmkataba wa amani na serikali ya Sudan Kusini huko Khartoum, Sudan, Juni 27, 2018. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Sudan Kusini, nchi changa duniani inaendelea kukabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, kwa mujibu wa mpatanishi wa Sudan.

"Makundi makubwa ya upinzani nchini Sudan Kusini, ikiwa ni pamoja na SPLM-IO (la Riek Machar), wamekataa kutia saini waraka wa mwisho, na kudai waache wazi sehemu yao ya kutia saini," amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Al-Dirdiry Ahmed, ambaye nchi yake inashiriki mazungumzo ya amani nchini Sudan Kusini.

Rais Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar walitia saini makubaliano ya Khartoum tarehe 5 Agosti na kusisitiza kurejea nyumbani kwa Machar ili kushikilia moja ya nafasi tano za makamu wa rais katika serikali ya umoja wa kitaifa. Bw Machar alilazimika kukimbilia nje ya nchi baada ya mapigano mabaya yaliyosababisha vifo vingi mnamo Agosti 2016.

Kufuatia makubaliano yao juu ya kugawana madaraka, wadau katika mazungumzo hayo walikubali kuendelea na mazungumzo huko Khartoum hadi kusainiwa kwa mkataba wa mwisho wa amani.

"Hakutakuwa na amani nchini Sudan Kusini wakati makundi (ya upinzani) hayatotia saini " waraka huo, waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan alionya, huku akisisitiza kuwa mazungumzo hayo ni ya mwisho kufanyika mjini Khartoum ".

Kwa mujibu wa waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, wapatanishi watawasilisha waraka kwa nchi wanachama wa Afrika Mashariki ambao wamekuwa wakita kwa miezi kadhaa ili kuanzisha mchakato wa amani nchini Sudan Kusini.

Sudan Kusini imepata uhuru wake kutoka mikononi mwa Sudan tangu mwaka 2011 lakini ilitumbukia katika vita mnamo mwezi Desemba 2013 kufuatia uhasama kati ya Salva Kiir na Riek, na hivyo kusababisha vifo vya watu wengi, huku watu milioni nne wakikimbilia nchi jirani na katika maeneo mbalimbali ya nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.