Pata taarifa kuu
UGANDA-USALAMA-SIASA-HAKI

Wakili wa mbunge Bobi Wine azuiwa kuingia Uganda

Wakili wa kimataifa wa mbunge wa Kyadondo Mashariki na mwanamuziki, Robert Kyagulanyi, anayefahamika kwa jina la Bobi Wine, amezuiwa kuingia nchini Uganda, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Mwanamuziki na mwanasiasa Bobi Wine wakati wa maandamano huko Kampala Julai 11, 2018.
Mwanamuziki na mwanasiasa Bobi Wine wakati wa maandamano huko Kampala Julai 11, 2018. Isaac Kasamani / AFP
Matangazo ya kibiashara

Robert Amsterdam, raia kutoka Canada, alikuwa miongoni mwa mawakili waliokuwa wameorodheshwa kumtetea Bw Kyagulanyi katika kesi ya uhaini inayomkabili.

Kwenye gazeti la The Guardian, Bw Amsterdam alitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuwawekea vikwazo watu wanaohusika katika ukiukaji wa haki za kibinadamu nchini Uganda.

Taarifa kutoka kwa baadhi ya vyombo vya habari nchini Uganda zinazema kuwa Robert Amsterdam ameorodheshwa kama mtu asiyetakikana nchini Uganda na serikali ya nchi hiyo.

Bobi Wine anaendelea kuzuiliwa jela katika gereza la Gulu pamoja na baadhi ya wabunge na watu wengine zaidi ya 20.

Anashtumiwa kuhusika katika vurugu za kurushia mawe magari ya msafara wa rais Yoweri Kaguta Museveni wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Arua.

Wiki iliyopita, Bobi Wine aliachiliwa huru na kukamatwa na Jeshi la polisi, muda mfupi baada ya mahakama ya kijeshi kutoa uamuzi wa kumuachilia huru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.