Pata taarifa kuu
KENYA-UFISADI-UCHUMI

Vita dhidi ya ufisadi yaendelea Kenya

Washukiwa 48 wanaodaiwa kuhusika katika kashfa ya ufisadi katika Shirika la huduma kwa vijana nchini Kenya, NYS, wanatarajiwa kukamatwa na kushtakiwa wiki hii.

Wakati wa Uhuru Kenyatta, aliahidi kupambana na maafisa wafisadi kwenye serikali yake.
Wakati wa Uhuru Kenyatta, aliahidi kupambana na maafisa wafisadi kwenye serikali yake. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi wa mkaguzi wa matumizi ya fedha za serikali, umebaini kuwaa Dola Milioni 80 zilitoweka katika mazingira yasiyoeleweka.

Ofisi ya kiongozi wa mashataka nchini humo imepokea faili 10 kuhusu washukiwa wa kashafa hiyo.

Waziri wa Masuala ya umma, vijana na jinsia  Margaret Kobia siku ya Jumatatu aliwapa likizo ya lazima maafisa kadhaa wa shirika hilo.

Kati ya waliaogizwa kufanya hivyo ni wasimamizi wa idara za ununuzi na uagizaji, fedha na uhasibu. Haya yamejiri siku chache tu baada ya rais Uhuru Kenyatta kupokea barua za kujiondoa kwa Katibu mkuu wa wizara hiyo ya Vijana Lilian Omollo na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo ya NYS Richard Ndubai ili uchunguzi uendelezwe kwa njia rahisi.

Kujiondoa kwa wawili hawa ili kuruhusu Idara ya upelelezi wa jinai na tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC kukamilisha uchunguzi wake dhidi ya sakata ya NYS ambayo imeitikisa serikali ya rais Uhuru Kenyatta kwa mara nyingine, kumeibua masuali mengi ya jinsi fedha za umma zimedaiwa kufujwa mara kwa mara na taasisi hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.