Pata taarifa kuu
BURUNDI-BBC-VOA-VYOMBO VYA HABARI

Matangazo ya BBC na VOA yapigwa marufuku Burundi

Serikali ya Burundi imeonya na kuchukua hatua ya kupiga marufuku matangazo ya mashirika ya utangazaji ya BBC na VOA kwa muda wa miezi sita kuanzia Mei 7 mwaka huu.

Burundi inajitayarisha kwa kura ya maoni Mei 17 ambayo huenda ikamuongezea muda wa kuhudumu rais Pierre Nkurunziza hadi mwaka 2034.
Burundi inajitayarisha kwa kura ya maoni Mei 17 ambayo huenda ikamuongezea muda wa kuhudumu rais Pierre Nkurunziza hadi mwaka 2034. © RFI-KISWAHILI
Matangazo ya kibiashara

Mashirika haya ya utangazaji yanashtumiwa na serikali ya Burundi kutofuata sheria zinazotoa muongozo wa uandishi habari nchini.

Serikali ya Burundi naishutumu BBC kwa kushindwa kumwajibisha mwanaharakati wa Burundi katika mahojiano aliyofanyiwa katika idhaa ya kifaransa ya shirika hilo.

Mtandao wa habari unaoegemea upande wa serikali ya Burundi, Ikiriho, kwenye ukurasa wake wa Twitter, umerusha nyaraka ya taarifa hiyo.

Radio kadhaa za kibinfasi zimeharibiwa na kufungwa nchni humo wakati wa mzozo wa kisiasa ulioanza mnamo 2015, wakati rais Nkurunziza aliposhinda muhula wa tatu madrakani, uliozusha mgogoro wa kisiasa na kusababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine kuyahama makazi yao. Watu zaidi ya 3000 wamezuiliwa katika jela mbalimbali kwa mujibu wa mashirika ya kiraia nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.