Pata taarifa kuu
RWANDA-WAISLAMU-MISIKITI

Rwanda yapiga marufuku matumizi ya adhana misikitini jijini Kigali

Serikali ya Rwanda imepiga marufuku adhana au wito kwa Waislamu kuhudhuria maombi  katika baadhi ya maeneo ya jiji kuu Kigali.

Picha ya jengo la Msikiti jijini Kigali
Picha ya jengo la Msikiti jijini Kigali AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya serikali kufunga Makanisha zaidi ya 700 kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na eneo dogo la kufanyia ibada na masuala ya usafi.

Eneo linaloathirika zaidi na hatua hiyo ya serikali ni lile la Nyarugenge linaloelezwa kuwa na misikiti mingi.

Uamuzi huu wa serikali ya Kigali, umewakera viongozi wa dini ya Kiislamu nchini humo ambao wamesema ni kuminya uhuru wa kuabudu nchini humo.

Sheikh Salim Hitimana, kiongozi wa Baraza la Waislamu nchini humo amesema hatua hiyo ya serikali imewashangaza sana.

Hata hivyo, ameongeza kuwa watazungumza na viongozi wa serikali na kutoa mtazamo wao kabla ya kutoa msimamo wa mwisho.

Kigali imekuwa ikisema kuwepo kwa makanisa na misikiti mingi katika jiji kuu, inahatarisha usalama na uchafuzi wa mazingira hasa kutokana na sauti kubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.