Pata taarifa kuu
WAKIMBIZI-BURUNDI-DRC-RWANDA

Wakimbizi wa Burundi waliokuwa wanaishi DRC, wakimbilia Rwanda

Wakimbizi kutoka Burundi wapatao 2,500 waliokuwa wanaishi katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamekimbilia nchini Rwanda kwa hofu ya kurudishwa kwa nguvu nchini mwao.

Kambi ya  Mahama nchini Rwanda  iliyotoa hifadhi kwa wakimbizi kutoka Burundi
Kambi ya Mahama nchini Rwanda iliyotoa hifadhi kwa wakimbizi kutoka Burundi Philip Kleinfeld
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Rwanda imethibitisha kuwasili kwa wakimbizi hao ambao pamoja na hofu ya kurudishwa Burundi, wamekataa kusajiliwa kupitia mitambo ya kieletroniki ili kutambuliwa rasmi.

Wakimbizi hao wanasema hawawezi kusajiliwa kwa mitambo hiyo kwa sababu ya imani yao ya dini.

Wakimbizi zao wanaoongozwa na nabii wa kike anayefahamika kwa jina la Zebiya.

Aidha, wamekuwa wakisema wamekimbia nchi yao kwa sababu wamekuwa wakiteswa kwa sababu ya imani yao.

Mwezi Januari, Mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu ilikataa kuwapa mahitaji muhimu ya kibinadamu kama chakula na dawa baada ya kukataa kusajiliwa.

Mwezi Septemba mwaka 2017, wakimbizi 36 wa Burundi waliuawa baada ya makabiliano na maafisa wa usalama wa DRC, wakati wakiandamana kulalamikia kuzuiwa kwa wenzao katika kambi ya Kamanyola.

Maelfu ya raia wa Burundi wamekimbia nchi yao kwa tangu mwaka 2015 kwa sababu za kisiasa na kwenda katika nchi jirani kama Rwanda, DRC, Tanzania na Uganda.

Rais Pierre Nkurunziza amekuwa akitoa wito kwa wakimbizi hao kurejea nyumbani kwa kile anachosema usalama umerejea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.