Pata taarifa kuu
TANZANIA

Tanzania: Wanaume 12 wakamatwa kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Polisi nchini Tanzania inawashikilia wanaume 12 wakiwemo raia wawili wa Afrika Kusini na mmoja wa Uganda kwa tuhuma za kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja katika operesheni inayoendelea dhidi ya ushoga.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania. Issa Michuzi
Matangazo ya kibiashara

Kamanda wa polisi wa jiji la Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kwenye hoteli ya Peacok wakiwa wanahamasisha mapenzi ya jinsia moja.

Mambosasa amesema wanaume 12 wanaendelea kuhojiwa kabla ya kupelekwa mahakamani licha ya kutosema ni lini watu hao walikamatwa.

Kamanda mambo sasa amesema “sheria za Tanzania zinakataza uhusiano wa kimapenzi wa watu wa jinsia moja, kufanya hivi ni kinyume cha sheria za Tanzania’.

Miongoni mwa waliokamatwa kwa mujibu wa kamanda Mambosasa ni pamoja na meneja wa Hotel aliyeruhusu kutoa ukumbi kwa watu hao.

Kamanda Mambosasa ametoa wito kwa raia kutoa taarifa kwa Polisi pale wanapoona au kuhisi kuna watu wanahamasisha vitendo vya ushoga.

Mwezi mmoja uliopita watu 20 walikamatwa visiwani Zanzibar katika operesheni kama hii inayoendeshwa Tanzania bara.

Mwezi Februari mwaka huu nchi ya Tanzania ilijikuta ikikoslewa vikali na hasa na taifa la Marekani ambapo ilitangaza kufunga vituo kadhaa vya utoaji wa elimu na dawa kwa waathirika wa virusi vya UKIMWI, Tanzania ikisema vituo hivi vilikuwa vinatumiwa kuhamasisha ushoga.

Tanzania pia imesema itawarudisha nchini mwao raia wote wa kigeni watakaobainika kuhamasisha ushoga.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania mtu anayepatikana na hatia ya kujihusisha na mapenzi ya jinsi moja adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela lakini hata hivyo hakuna sheria inayokataza mapenzi ya jinsia moja kwa wanawake.

Mwaka 2014 nchi ya Uganda ilijaribu kuweka adhabu ya kifo kwa watu watakaokamatwa wakijihusisha na mapenzi ya jinsia moja, sheria ambayo ilikosolewa vikali na baadae kubadilishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.