Pata taarifa kuu
Tanzania-USALAMA

Tundu Lissu asafirishwa Nairobi kupata matibabu

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania na rais wa chama cha Mawakili cha Tanganyika Tundu Lissu, amesafirishwa jijini Nairobi nchini Kenya kwenda kupata matibabu zaidi.

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu
Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu youtube
Matangazo ya kibiashara

Lissu alipigwa risasi siku ya Alhamisi na watu waisofahamika akiwa ndani ya gari lake nyumbani kwake mjini Dodoma.

Tukio hili limelaaniwa huku serikali kupitia Waziri wa Usalama wa ndani Mwigulu Nchemba akisema kuwa maafisa wanaendeleza uchunguzi kuwakamata na kuwashitaki waliousika na tukio hilo.

Siku ya Alhamisi kiongozi wa chama hicho Freeman Mbowe a;lisema, Lissu anaendelea kupata matibabu ya dharura lakini hali yake sio nzuri.

Tundu Lissu amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya rais John Magufuli na hata amekuwa akimwita “Dikteta”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.